Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

MSD Yakabidhi Jenereta la Kisasa Hospitali ya Lushoto na Muheza
Aug 09, 2023
MSD Yakabidhi Jenereta la Kisasa Hospitali ya Lushoto na Muheza
Muonekano wa jenereta za kisasa lililokabidhiwa na Bohari ya Dawa (MSD) kwenye Hospitali za Wilaya ya Lushoto na Muheza.
Na Na Mwandishi Wetu

Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi Jenereta za kisasa kwenye Hospitali za Wilaya za Lushoto na Muheza.

Jenereta hizo zimekabidhiwa hivi karibuni ikiwa sehemu ya maombi ya hospitali hizo kwa MSD zikiwa na lengo la kuboresha huduma kwa wananchi.

Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya ya Lushoto, Dkt. Godfrey Andrew  ameishukuru Serikali  kwa hatua ya maboresho ya sekta ya afya na kueleza kuwa jenereta hilo  litawezesha baadhi ya huduma kufanyika hata pale ambapo umeme wa kawaida utakuwa umepata hitilafu.

Kwa upande wake Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza, Nuru Kionywaki amesema huduma za MSD zimekuwa na uhakika kwani ni kipindi kifupi toka hospitali imeagiza jenereta hilo na sasa limekabidhiwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi