Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mradi wa Ujenzi wa Meli Mpya na Chelezo Washika Kasi
Nov 01, 2019
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_48492" align="aligncenter" width="750"] Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Bw. Eric Hamissi akimpa maelezo Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi hatua iliyofikiwa ikiwemo vifaa ambavyo vimeshawasili nchini mpaka sasa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya kubwa ya abiria ambapo Serikali imeweka Kiasi cha Shilingi Bilioni 89 katika mradi huu.[/caption]

Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi jana (Oktoba 31) alitembelea  mradi wa ujenzi wa meli ya kisasa ambayo ni meli kubwa kuliko zote katika Ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na ujenzi wa chelezo kwa ajili ya matengenezo na marekebisho ya meli mbalimbali ikiwa ni uwekezaji unaofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais  Dkt. John Pombe Magufuli.

Akiwa katika eneo hilo,  Dkt. Abbasi alisema kuwa ujenzi wa meli  mpya ni ahadi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 23 iliyopita,  ambayo imetekelezwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais . Dkt Magufuli.

[caption id="attachment_48493" align="aligncenter" width="750"] Meneja Mradi wa Chelezo na Ukarabati wa Meli za MV. Victoria na MV Butiama Mhandisi Abel Gwanafyo akimpa maelezo Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Chelezo ambayo ni sehemu kubwa itakayokuwa inapaki meli kwa ajili ya matengenezo na marekebisho mbalimbali, Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Bw. Eric Hamissi[/caption] [caption id="attachment_48495" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Mafundi wakiendelea na zoezi la uunganishaji wa vyuma kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya kubwa ya abiria itakayofanya kazi katika ziwa victoria.[/caption]

Aidha, Dkt. Abbasi aliongeza kuwa ujenzi wa meli  mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1, 200 umefikia  asilimia 33 ya ujenzi na utakamilika mapema mwaka 2021, ambapo Serikali imewekeza zaidi ya TZS Bilioni 150, kwenye mradi ya meli pamoja na ujenzi wa chelezo.

Aidha, Dkt. Abbasi alishuhudia ukarabati unaoendelea katika meli ya MV. Victoria, ambayo baada ya kukamilika itasaidia  kutoa huduma bora za usafiri kwenye eneo la Ziwa Victoria.

Vilevile,  akiwa ziarani hapo Dkt.  Abbasi alisema kuwa ipo miradi mingi kwenye eneo la Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika, inatakayo gharimu  zaidi ya TZS Bilioni 300.

Aliongeza kuwa hivi karibuni, Serikali itasaini makubaliano ya utekelezaji  wa miradi  ya ujenzi wa  meli katika eneo la Ziwa Tanganyika na uundaji wa meli 3  mpya na za kisasa katika eneo la Ziwa Nyasa.

  [caption id="attachment_48496" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Mafundi wakiendelea na zoezi la uunganishaji wa vyuma kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya kubwa ya abiria itakayofanya kazi katika ziwa victoria.[/caption] [caption id="attachment_48497" align="aligncenter" width="750"] Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wakandarasi wanaojenga meli mpya na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli alipotembelea eneo hilo ili kujionea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa meli hiyo itakayofanya kazi katika ziwa victoria.[/caption]

Akitaja, meli zilizokamilika kutokana na utekelezaji wa ahadi za Serikali hadi sasa kuwa ni meli za mbili za mizigo za MV. Ruvuma,  na meli kubwa ya kisasa ya abiria ya MV. Mbeya II na ambayo tayari imeanza kazi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Eric Hamissi,  alisema kuwa ujenzi  wa meli hiyo mpya unaendelea vizuri, na Septemba 30, mwaka huu vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa vilianza kuletwa na sasa kazi ya uunganishwaji wa vyuma imeshaanza.

Aliongeza kuwa, ujenzi wa chelezo umefikia 53%, na ifikapo Machi mwakani chelezo itanza kutumika kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya.

Aidha, Bw. Hamissi alisema anaishukuru Serikali kwa ujenzi miradi hii  miwili pamoja na ya  ukarabariti wa MV.  Butiama na MV.  Victoria inayoendelea kwani itaigharimu Serikali TZS Bilioni 150, na hadi sasa Serikali imeshatoa TZS Bilioni 70.8, sawa na 47% ya miradi yote minne.

[caption id="attachment_48498" align="aligncenter" width="750"] Muonekano wa Meli ya MV. Victoria inayokarabatiwa na Kampuni ya Huduma za Meli.[/caption] [caption id="attachment_48499" align="aligncenter" width="750"] Muonekano wa Chelezo inayojengwa na Kampuni ya Huduma za Meli ambayo ni sehemu kubwa itakayokuwa inapaki meli kwa ajili ya matengenezo na marekebisho mbalimbali ambayo imefikia asilimia 53 ya ujenzi na itaanza kutumika mwezi Machi 2020[/caption]

Bw. Hamissi,  aliongeza kuwa miradi hii imesaidia kukuza uchumi wa Mwanza kwa kutoa ajira zaidi ya watu 1,000 pamoja utumiaji wa malighafi na watoa huduma, hali inayosaidia kuboresha maisha ya wananchi.

Alifafanua kuwa,  huu ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ambao haujawahi kutokea  tangu Uhuru na  ni mapinduzi  katika usafiri wa njia ya maji kwa kutekeleza miradi mikubwa minne kwa wakati mmoja, na kuwa awali meli nyingi zilijengwa kwa msaada mfano MV. Sangara.

Naye, Li Yonjee, Mtaalamu wa Meli kutoka Korea Kusini, alisema anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwapa fursa ya kushiriki katika uundaji wa meli mpya ya kisasa,  watatumia ujuzi wao wa uundaji wa meli waliofanya katika nchi za Korea ya Kusini,  China na Japan,  zikiwa ndio nchi kubwa za uundaji wa meli duniani,  katika kuunda meli mpya ya Tanzania.

Vilevile,  Bw. Li alisema kuwa wanaahidi kutimiza matarajio ya Serikali na watanzania kwa ujumla kwa  kuunda meli hiyo kwa mafanikio,  pamoja kuikamilisha kwa wakati.

Aidha, Bhoke Siguta mwanamke anayefanyakazi ya kuchomelea vyuma katika mradi wa uundaji wa meli mpya, alisema anaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutekeleza miradi mbalimbali inayogusa  maisha ya watanzania, ikiwemo kutoa ajira.

Bi. Siguta alisisitiza kuwa, kupitia mradi huu wa uundaji wa meli mpya ameweza kupata ajira,  inayompatia kipato cha kumsaidia kutunza familia yake.

Pia,  ameshauri wanawake kujishughulisha na kazi za uchomeleaji vyuma,  kwani ni kazi nzuri na zitawajengea uwezo zaidi wa kujiamini pamoja na kukuza kipato.

Awali,  Dkt. Abbasi alikutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya Huduma za Meli kuhusu mikakati na maboresho ya kampuni hiyo.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi