Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (Mwenye Miwani) akioneshwa eneo la
kiwanda cha nyama Shinyanga na Mkurugenzi wa Ubinafsishaji na
Ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Jones
Mwalemba (aliyenyoosha mkono) kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uzalishaji
Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Asimwe Lovince kushoto
kwake ni Mwenyekiti wa Wilaya a shinyanga wa CCM.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametoa siku saba kwa wawekezaji
wa kiwanda cha nyama Shinyanga cha Kampuni ya Triple S Beef Limited na
Agri Vision kuwasilisha hati zote za umiliki hati ya eneo la kiwanda na
eneo la kuhifadhia mifugo baadha ya kushindwa kukiendeleza kwa miaka 11.
Akizungumza katika kiwanda hicho leo Mpina amuagiza Mkurugenzi wa
Ubinafsishaji na Ufuatiliaji Jones Mwalemba kutoka Hazina kuhakikisha
kwamba ifikapo Juni 30 mwaka huu kiwanda hicho kiwe kimempata mwekezaji
ambaye ataanza kazi mara moja ya uchinjaji ili kutoa ajira na
kuliingizia taifa mapato.
Aidha amemuagiza Msajili wa Hazina kuanza uhakiki wa mali zote za
kiwanda hicho baada ya kubainika wizi uliokithiri katika kiwanda hicho.Pia Mpina ameamuru mmliki wa Kampuni inayolinda kiwanda hicho kukamatwa
mara moja na kufikishwa katika mikono ya sheria kwa ajili ya kujibu
mashitaka wa wizi wa mali za kiwanda hicho ambapo amemtaka Mkuu wa
Mkoa kuhakikisha kuanzia sasa kiwanda hicho kilindwe na vyombo vya
Serikali badala ya makampuni binafsi.
Waziri Mpina alisema hatua ya Kampuni ya Triple S kuuza kiwanda na
kuingia mkataba mpya na Kampuni ya Agrovisioni ni kinyume na mkataba
wa awali ilioingia na Serikali.“Huu ni ukiukwaji wa masharti ya Mkataba kulingana na kifungo cha 16.1
ambapo sasa kinauondoa umiliki wake katika kiwanda hiki” alisisitiza
MpinaMkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt.
Lovince Asimwe kiwanda kilianza ujenzi wake mwaka 1975 na kwamba
kimegharimu dola za kimarekani milioni tatu na kilijengwa na Serikali
kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
Alisema mwaka 2007 kiwanda hicho kilibinafsishwa kwa mwekezaji Tripple S
Beef Limited lakini kutoka na na matatizo ya uendeshaji kiwanda hicho
kilifungwa mwaka 2017 na kukabidhiwa kwa Serikali.