[caption id="attachment_16717" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga kwenye Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Morogoro leo.[/caption]
Na: Sebera Fugence – WCF, Morogoro
Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya waajiri ambao hawajajisajili katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Mhe. Biswalo Mganga katika mafunzo ya uelimishaji wa Mawakili wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofanyika Mkoani Morogoro leo.
Mhe. Mganga alisema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa waajiri watakaobainika kutenda makosa mengine yakiwemo ya kutowasilisha michango katika Mfuko kwa wakati.
[caption id="attachment_16720" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Bw. Mashtaka Biswalo Mganga akifungua Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Morogoro leo.[/caption]Alisema lengo la Serikali ni kuona kila mfanyakazi anayeumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi anapata mafao yake kama ambavyo imeeekezwa katika Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 ikisomwa pamoja na kanuni zake za mwaka 2016.
“Mafunzo haya yatatoa fursa kwa Ofisi yangu na Maafisa wengine kueleza uzoefu wao kuhusu namna ya kuendesha Mashauri ya Jinai zikiwemo changamoto wanazokutana nazo na mapendekezo ya utatuzi wa changamoto hizo hasa pale wanaposhughulikia kesi dhidi ya waajiri wanaokiuka sheria” alisema Mhe Mganga.
Aliongeza kuwa Ofisi yake ni mdau muhimu sana katika kuhakikisha kuwa matakwa ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi yanatekelezwa kikamilifu na wale wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.
[caption id="attachment_16723" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga akifungua Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Morogoro leo.[/caption] [caption id="attachment_16724" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga (wa nne kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Morogoro leo.[/caption]Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) nchini Bw. Masha Mshomba alisema Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ipo kwa mujibu wa Sheria ya Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na moja kati majukumu yake ya msingi ni kufungua, kusimamia na kuendesha mashauri ya jinai katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Alisema Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ni mdau muhimu sana katika kuhakikisha malengo ya Mfuko huo yanafikiwa kwani ndio wasimamizi wakuu katika uendeshaji mashauri ya jinai yakiwemo makosa ya jinai yaliyoainishwa kwenye Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Aliitaja changomoto inayoikabii Mfuko huo kuwa ni idadi kubwa ya waajiri ambao hawajajisajili na hawachangii kwenye Mfuko na kuongeza kuwa changamoto hiyo isipopatiwa suluhisho la haraka itaathiri uwezo wa Mfuko kulipa fidia kwa wafanyakazi.
[caption id="attachment_16726" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mashtaka katika Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Morogoro leo. (Picha zote na Mpiga picha wetu)[/caption]Alisema hadi kufikia juni 30, 2017 Mfuko umelipa fidia ya kiasi cha Shilingi 613,843,555.64 ikiwa ni gharama za matibabu fidia ya ulemavu wa muda mfupi na ulemavu wa kudumu.
Kwa upande wa usajili Bw. Mshomba amesema hadi kufikia juni 30, 2017 mfuko tayari ulikuwa umesajii waajiri 7,857 ambapo hadi kufikia juni 31, 2017 inakadiriwa kuwa zaidi ya waajiri 13,918 waliopo Tanzania Bara hawajasajiiwa kwenye Mfuko.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iiyoanzishwa chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 marejeo ya mwaka 2015 kwa lengo la kushughuikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi wanaoumia ama kuugua ama kufariki wakati wakitekeeza majukumu ya mwajiri kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.