Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Mhariri Mtendaji wa TSN Watembelea Banda la EWURA Katika Maonesho ya Sabasaba
Jul 04, 2017
Na Msemaji Mkuu

 

2

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dk. Hassan Abbasi akisalimiana na Meneja Mwasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) wakati alipotembelea banda hilo akiwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya hiyo kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya J.K.Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Maonyesho hayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje (TANTRADE), katika picha ni baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

1

Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz akisalimiana na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) Bw. Titus Kaguo wakati alipotembelea banda hilo akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dk. Hassan Abbasi kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya J.K.Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Maonyesho hayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje (TANTRADE) na yanafanyika kilwa mwaka mwezi Julai.

3

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) Bw. Titus Kaguo akitoa maelezo kwa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz kushoto na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dk. Hassan Abbasi wakati walipotembelea katika banda hilo.

4

Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz akisaini kitabu cha wageni katika banda hilo.

5

Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz akiagana na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) Bw. Titus Kaguo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dk. Hassan Abbasi (kushoto) mara baada ya kutembelea katika banda hilo , katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Rodney Thadeus.

6

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) Bw. Titus Kaguo kushoto pamoja na wafanyakazi wenzake wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi