Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

MKURABITA yaleta ukombozi Mufindi kupitia hatimiliki za kimila
Jan 26, 2021
Na Msemaji Mkuu

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njolai akisisitiza umuhimu wa Halmashauri zote hapa nchini kuiga mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kwa kutekeleza kwa vitendo dhana ya urasimishaji ardhi unaowawezesha wananchi kupata hatimilki za kimila za kumiliki ardhi zinazotolewa kufuatia MKURABITA kujenga uwezo kwa Halmashauri hiyo na kuiwezesha kuendelea na kazi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na pia kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kazi hiyo, hayo yamejiri  katika Kijiji cha Lugodalutali Kata ya Igombavanu, Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambapo ilikabidhihati 342 kwa wananchi wa Kijiji hicho.

Na Mwandishi Wetu- Mufindi

Hatimilki za kimila za kumiki ardhi 342 kati ya 800 zilizoandaliwa zimetolewa kwa Wananchi wa kijiji cha Lugodalutali Kata ya Igombavanu, Halmashauri ya hilaya ya Mufindi mkoani Iringa kuwawezesha wananchi hao kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza wakati akikabidhi Hati hizo  leo Januari 25, 2021, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel ole Njoolay amesema utoaji hati hizo uwe chachu kwa halmashuri nyingine hapa nchini kuiga mfano wa wilaya ya Mufindi ambayo imefanikiwa katika urasimishaji ardhi kwa kiwango kikubwa baada ya kujengewa uwezo na MKURABITA.

“Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi umefanikiwa katika kuendeleza dhana ya urasimishaji kwa vitendo kwa kutenga fedha za ndani na kushirikisha wadau waliochangia katika kufanya suala la urasimishaji kuwa endelevu kwa wananchi wa Wilaya hii”, amesisitiza Mhe. Njoolay.

Katika ufafanua wake, Njoolay amesema urasimishaji umewezesha wananchi kupata hatimilki ambazo zinawawezesha kupanua wigo wa shughuli za uzalishaji na kukuza vipato vyao na Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe.Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njolai akikabidhi hatimilki za kimila za kumiliki ardhi kwa mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Lugodaluli wilayani Mufindi baada ya MKURABITA kujenga uwezo kwa Halmashauri hiyo na kuiwezesha kuendelea na kazi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na pia kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya mpango wa urasimishaji ardhi vijijini ikiwemo mashamba ya chai.

Akieleza faida za urasimishaji kwa wananchi hao Mhe. Njoolay amesema kuwa ni pamoja na kusaidia katika utunzaji wa mazingira, kulindwa kisheria kwa maeneo yote yalipimwa,kuepusha migogoro ya ardhi na kuwawezesha wananchi kupata mikopo katika taasisi za fedha hivyo kukuza shuguli za uzalishaji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe. Jamhuri William amesema urasimishaji katika wilaya hiyo umeleta tija kubwa na umewezesha kutambuliwa kwa maeneo zaidi ya 1700 ya vyanzo vya maji na hivyo kuwekewa mkakati wa kuyalinda kwa manufaa ya Taifa na wananchi wa Wilaya hiyo.

Mratibu wa MKURABITA,  Dkt. Seraphia  Mgembe akieleza faida za hatimilki za kimila za kumiliki ardhi katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi na hivyo kuondokana na umasikini.

Aliongeza kuwa mashamba zaidi ya 2600 yamepimwa  na kuwezesha kupungua kwa migogoro ya ardhi kwa kiwango kikubwa.

Naye Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe amewaasa wananchi waliopokea hati hizo kuhakikisha wanazitumia kuleta mageuzi ya kuchumi kwa kuimarisha shughuli zao ili kuongeza tija na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Sehemu ya wananchi walioshiriki katika hafla ya utoaji hatimilki za kimila za kumiliki ardhi katika Kijiji cha Lugodalutali Kata ya Igombavanu, Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njoolay kabla ya kuwakabidhi hati 342.

“Ukuaji wa uchumi unaenda sambamba na urasimishaji ardhi kwa wananchi ili kufungua zaidi fursa za kiuchumi kwa kuwa Taasisi za fedha ziko tayari kuwawezesha kwa kutumia hati hizo,” alisisitiza Dkt. Mgembe.

Akieleza zaidi Dkt. Mgembe amesema kuwa hati hizo zitawawezesha wananchi kuingia ubia katika uwekezaji wa miradi mbalimbali inayolenga kuleta maendeleo.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa ya Halmashauri ya Wilaya hiyo zaidi shilingi milioni 429,840,000/ zimekopeshwa kwa wananchi kupitia hatimilki za kimila za kumiliki ardhi zilizotolewa baada ya urasimishaji ardhi katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa Mhe. Jamhuri William, akiwaeleza wananchi faida za utunzaji wa mazingira baada ya urasimishaji ardhi katika Kijiji cha Lugodalutali Kata ya Igombavanu, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi baada ya wananchi wa kijiji hicho kupokea hatimiliki za kimila za ardhi  342 walizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njoolay leo Januari 25,2021.

Hati zilizotolewa tangu kuanza kwa urasimishaji katika Wilaya hiyo ni 6,798 zikihusisha wananchi wa vijiji 28 vilivyonufaika na urasimishaji uliofanyika kwa kushirikiana na wadau baada ya Halmashauri hiyo kujengewa uwezo na MKURABITA.

Aidha vijiji 113 vimepimwa mipaka yake kati 121 na vijiji 52 vimeandaliwa mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Mmoja wa wanufaika wa hatimilki za kimila za kumiliki ardhi katika Kijiji cha Lugodalutali Kata ya Igombavanu, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Bw. Hassan Lugenge akitoa neno la shukrani  kwa MKURABITA na kueleza  faida za hati hizo ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njoolay leo Januari 25,2021 alikabidhi hati 342 kwa wananchi wa Kijiji hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njoolay (wanne kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja wajumbe wa Kamati hiyo, Viongozi mbalimbali wa MKURABITA na  wale wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa pamoja  na wananchi wa Kijiji cha Lugodalutali Kata ya Igombavanu baada ya wananchi hao kukabidhiwa hatimilki za kimila za kumiliki ardhi kama zinavyoonekana.
Mratibu wa MKURABITA,  Dkt. Seraphia   Mgembe (wa kwanza kulia) akifurahia ngoma na wananchi wa Kijiji cha Lugodalutali Kata ya Igombavanu baada ya kukabidhiwa hatimilki za kimila za kumiliki ardhi baada ya MKURABITA kuijengea uwezo Halmashauri ya Wilaya hiyo.
 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi