Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

MKURABITA Yaleta Neema kwa Wananchi Wilayani Mpwapwa
Feb 04, 2020
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_50668" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Capt. Mstaafu George Mkuchika akimpongeza mkazi wa kijiji ya Inzovu wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma Bw.Yohana Yaredi Mogoile kabla ya kumkabidhi hatimilki ya kimila ya kumiliki ardhi mkazi huyo wakati wa hafla ya kukabidhi hati hizo baada ya zoezi la urasimishaji ardhi kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), hayo yamejiri Januari 1, 2020.[/caption]

Na  Mwandishi Wetu-Mpwapwa

Serikali itaendelea kuwawezesha  wananchi kujikwamua kiuchumi kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Inzovu wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wakati akikabidhi hati kwa wananchi walinufaika na mpango huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. Mstaafu George Mkuchika amesema kuwa dhamira ya Serikali kupitia mpango huo ni kuwawezesha wananchi kupitia hatimilki za kimila za kumiliki ardhi wanazopatiwa baada ya kurasimisha mashamba yao.

“ Mabenki yametuhakikishia kuwa yanawakopesha wananchi kupitia hatimilki za kimila za kumiliki ardhi zinazotolewa kwa wananchi baada ya kurasimisha mashamba yao kwa kuyapima na hivyo kuweza kujenga uwezo wa kujikwamua kiuchumi, wafanyabiashara wote wakubwa na wenye maduka wanakopa katika taasisi za fedha hivyo waliopata hati hizi zitumieni kujiletea maendeleo”, alisisitiza Waziri Mkuchika.

  [caption id="attachment_50669" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa akisisitiza umuhimu wa elimu kuhusu urasimishaji ardhi na faida zake kwa wananchi Wilayani Mpwapwa wakati wa hafla ya utoaji hati milki za kimila za kumiliki ardhi, baada ya zoezi la urasimishaji ardhi kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge  Tanzania (MKURABITA)na Halmashauri ya wilaya hiyo, hayo yamejiri Januari 1, 2020 ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. Mstaafu George Mkuchika alikuwa mgeni rasmi.[/caption]

Akifafanua amesema kuwa kuwepo kwa MKURABITA ni matokeo ya sera nzuri za Chama cha Mapinduzi zinazoelekeza katika kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa wananchi hasa wanyonge kwa kutumia rasilimali zilizopo katika maeneo yao ikiwemo ardhi.

Akitaja faida za urasimishaji ardhi Waziri Mkuchika amesema kuwa ni pamoja na kuondoa migogoro ya ardhi na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Kwa upande wake, Mratibu wa MKURABITA  Dkt. Seraphia Mgembe amesema kuwa mashamba 707 yalipimwa katika kijiji cha Inzovu huku 593 yakiwa ndiyo yenye sifa za kupatiwa hati milki za kimila za kumiliki ardhi.

“ Hati 159 zimeshaandaliwa na kutolewa kwa wananchi waliopo hapa na zilizobaki 434 tutahakikisha zinaandaliwa na zinawafikia walengwa kwa wakati tukishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa,s” alisisitiza Dkt. Mgembe

[caption id="attachment_50670" align="aligncenter" width="750"] Mratibu wa MKURABITA Dkt. Seraphia Mgembe akieleza hatua ziulizofikiwa katika kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi hatimilki za kimila za kumiliki ardhi, hayo yamejiri Januari 1, 2020.[/caption]

Akifafanua, Dkt. Mgembe amesema kuwa MKURABITA itashirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo katika kuwajengea uwezo wananchi wote walionufaika na urasimishaji ili waweze kutumia hati walizopata kujiletea maendeleo kupitia mafunzo yatakayoendeshwa kwa kushirikiana na taasisi za fedha yakiwemo mabenki na Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Aidha, Dkt. Mgembe aliahidi kuwa MKURABITA itahakikisha kuwa inajenga masjala ya kutunza hati katika kijiji hicho na kuwaasa wananchi kujitolea kushiriki katika kufanikisha kazi hiyo kupitia nguvu kazi yao.

Katika kuunga mkono jitihada za Serikali kuwawezesha wananchi Benki ya CRDB, TPB na NMB zimekuwa zikiwakopesha wananchi wenye hatimilki za kimila ili waweze kujiletea maendeleo na hivyo kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

[caption id="attachment_50671" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. Mstaafu George Mkuchika akiwa kwenye picha ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Inzovu wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma waliopatiwa hatimilki za kimila za kumiliki ardhi katika Kijiji hicho baada ya kurasimisha mashamba yao.[/caption] [caption id="attachment_50672" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka MKURABITA Bw. Mujungu Masyenene (Kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Urasimishaji Rasilimali na Biashara Bw. Japhet Werema (Kulia) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Capt. Mstaafu George Mkuchika wakati wa hafla ya utoaji hati milki za kimila za kumiki ardhi kwa wananchi wa Kijiji cha Inzovu wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_50673" align="aligncenter" width="750"] Mbunge wa jimbo la Mpwapwa Mhe. George Lubeleje akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia hatimilki za kimila za kumiliki ardhi katika kujiletea maendeleo ikiwemo kuzitumia kukopa katika taasisi za fedha yakiwemo mabenki.[/caption] [caption id="attachment_50674" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Inzovu Wilayani Mpwapwa wakiwa na hati milki za kimila za kumiliki ardhi baada ya kukabidhiwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Kapt. Mstaafu George Mkuchika wakati wa hafla iliyofanyika katika Kijiji hicho mwishoni mwa wiki.[/caption] [caption id="attachment_50675" align="aligncenter" width="750"] Wanafunzi wa Shule ya msingi Inzovu wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wakiimba wimbo wa kupongeza Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kuwezesha urasimishaji ardhi katika kijiji cha Inzovu wilayani humo.[/caption] [caption id="attachment_50676" align="aligncenter" width="750"] Kikundi cha ngoma kikionesha umahiri wake katika kucheza ngoma wakati wa hafla ya utoaji hatimilki za kimila za kumiki ardhi kwa wananchi wa Kijiji cha Inzovu Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_50677" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa Bi. Sara Komba akizungumza wakati wa hafla ya utoaji hatimilki za kimila za kumiki ardhi kwa wananchi wa kijiji cha Inzovu Wilayani humo.[/caption]

(Picha zote na Frank Mvungi)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi