Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

MKURABITA Yasaidia Kuondoa Migogoro ya Ardhi Wilayani Uyui
May 06, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_42782" align="aligncenter" width="900"] Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu akitoa elimu jana kwa wanakiji wa Kijiji cha Miyenze Wilayani Uyui Mkoani juu ya matumizi ya hati miliki za kimila walizopata kuboresha maisha yao.[/caption]

WANAKIJIJI  wa Kijiji cha Miyenze wilayani Uyui ambao wawezeshwa na Serikali kupitia Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) kwa kurasimisha maeneo yao na kupatiwa hati za hati miliki za kimila wameshauriwa kutafuta mikopo kwa ajili ya uboreshaji ufugaji wa kuku wa asili.

Kauli hiyo imetolewa jana na Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora Vincent Chacha wakati mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima na viongozi ambao wapewa hati miliki za kimila baada ya ardhi yao kupimwa na  kurasimishwa.

Alisema ni vema wakatumia ardhi zao zilizoramishwa katika kuendesha ufugaji bora wa mifugo iwemo wa kuku wa kienyeji ili kujipatia chakula , kipato na hivyo kuboresha maisha yao.

Chacha alisema ni vema wakatumia hati miliki za kimila walipata kutafua mitaji ambayo itawasaidia kujenga ujenzi wa mabanda ya kisasa ya ufugaji kuku, kununua mashine ya kutotoresha vifaranga na ununuzi wa chanjo na dawa mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa wa mdodo na ndui.

Alisema ikiwa wakulima hao wakizingatia utalaamu walipewa juu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji kisasa watapata fedha za haraka kwa kuwa ndio mifugo rahisi ya kufuga.

[caption id="attachment_42781" align="aligncenter" width="900"] Afisa Tafiti na Ufuatiliaji kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Francis Mjuni akitoa elimu jana kwa wanakijiji wa Miyenze wilayani Uyui waliopata hati miliki za kimila juu ya umuhimu wa utunzaji wa kumbukumbu katika shughuli mbali mbali.[/caption]

Chacha alisema soko la kuku wa kienyeji ni kubwa hivi sasa na liko karibu kutokana na Serikali kuhamia Dodoma.

Aidha Afisa Mifugo hiyo alisema Halmashauri ya Wilaya ya Tabora ina kuku wa kienyeji wapatao 876,000 na wanakusudia kuongeza idadi hiyo hadi kufikia milioni 1.2 ifikapo hapo mwakani.

Alisema wanatarajia kuanzisha wafugaji ambao wanakuwa walimu kwa wafugaji wengine kwenda kujifunza ufugaji kisasa na kwa tija.

Chacha alisema kwa sasa wameanza na shule za Msingi ili wafunzi wanaporudi kwao wawaelimisha wazazi wao juu ya ufugaji wa kisasa wa kuku wa kienyeji kwa ajili ya kuongeza kipato cha familia.

Naye Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakulima wote walipata hati ili waweze kutumia mtaji huo  kuboresha ufugaji wa mifugo ikiwemo kuku wa kienyeji.

Alisema pia wanapewa elimu ili waboreshe kilimo , utunzaji wa kumbukumbu za hesabu za kilimo na biashara na uandishi wa mpango wa biashara na uundaji wa vikundi vya uchumi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi