[caption id="attachment_48522" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Kepteni George Mkuchika akikata utepe kuzindua kampeni ya Utatu itawezekana na Mfumo wa kuripoti matukio ya rushwa (Takukuru App) uliofanyika katika Viwanja wa Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.[/caption]
Na. Mwandishi Wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utwala Bora, Kapteni, George Mkuchika amewataka wananchi kuiunga mkono Serikali katika kupambana na Rushwa ili kupunguza ajali za barabarani pamoja na kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wananchi.
[caption id="attachment_48523" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Kepteni George Mkuchika akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa kampeni ya Utatu itawezekana na Mfumo wa kuripoti matukio ya rushwa (Takukuru App) uliofanyika katika Viwanja wa Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.[/caption]Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya kuzuai rushwa barabarani Waziri Mkuchika amasema kuwa katika kampeni hiyo ijulikanayo kama “Utatu inayohusisha Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru, Jeshi la Polisi na Wananchi inawezekana na itasaidia katika kutoa taarifa za rushwa zishughulikiwe kwa haraka ili kupunguza ajali barabarani.
“ Nyote mtakubaliana na mimi kuwa jukumu la kupambana na rushwa lilikasimiwa kwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru, ili kukabiliana na vitendo vya Rushwa vinavypatikana katika maeneo yetu,kila mmoja wetu anapaswa kubeba jukumu la kupambana kama kampeni hii inavyoeleza”, alisema Waziri Mkuchika.
[caption id="attachment_48524" align="aligncenter" width="750"] Bendi ya Jeshi la Magereza likiongoza maandamano katika Uzinduzi wa kampeni ya Utatu itawezekana na Mfumo wa kuripoti matukio ya rushwa (Takukuru App) uliofanyika katika Viwanja wa Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_48525" align="aligncenter" width="750"] Askari kutoka jeshi la Usalama Barabarani wakionesha ukakamavu katika maandamano ya uzinduzi wa kampeni ya Utatu itawezekana na Mfumo wa kuripoti matukio ya rushwa (Takukuru App) uliofanyika katika Viwanja wa Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.[/caption]Alisema kuwa mara nyingi vitendo vya rushwa vinafanyika pale ambapo watu wanafanya kazi, wanafanya biashara, wanapata huduma na kwenye makazi kwa hiyo inawezekana kwa kila mtu kuchukua jukumu la kuzuia rushwa kwa sababu inatokea kwenye maeneo ambayo wananchi wanahusika,wanaisikia na kuona vitendo hivyo katika mazingira tofauti.
Waziri Mkuchika alieleza kuwa iwapo kila mtanzania atachukua dhamira ya dhati ya kuiunga mkono Serikali katika mapambano hayo, ajali za barabarani zitapungua, kwani mpaka sasa takwimu za mwaka 2018/2019 zinaonesha kuwa ajali za barabara zimepungua kwa kushirikisha wadau, Polisi na Taasisi ya kupambana na rushwa Takukuru.
[caption id="attachment_48526" align="aligncenter" width="750"] Wanafunzi kutoka Manispaa ya Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye maandamano ya uzinduzi wa kampeni ya Utatu itawezekana na Mfumo wa kuripoti matukio ya rushwa (Takukuru App) uliofanyika katika Viwanja wa Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_48527" align="aligncenter" width="750"] Msanii wa Mashairi ya kughani, Mrisho mpoto akitoa burudani katika uzinduzi wa kampeni ya Utatu itawezekana na Mfumo wa kuripoti matukio ya rushwa (Takukuru App) uliofanyika katika Viwanja wa Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.[/caption]Aidha Waziri Mkuchika amezindua Mfumo wa kitekenolojia unaoitwaTakukuru App unaopatikana kwenye simu ambao utatumika kuripoti vitendo vya Rushwa katika maeneo mbalimbali nchini.
“Mfumo huu ni mzuri kwani unamuwezesha mwananchi kukusanya taarifa na matukio ya vitendo vya rushwa kwa kutumia simu ya Mkononi na kuwasilisha kwa takukuru au jeshi la Polisi ambapo zitafanyiwa kazi na mtuhumiwa kufikishwa sehemu husika”, Alisema Waziri Mkuchika.
[caption id="attachment_48528" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Kepteni George Mkuchika akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Jeshi la Polisi, Viongozi wa Serikali na Wadau wa kupambana na Rushwa kutoka mashirika ya kimataifa, mara baada ya Uzinduzi wa kampeni ya Utatu itawezekana na Mfumo wa kuripoti matukio ya rushwa (Takukuru App) uliofanyika katika Viwanja wa Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_48529" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Kepteni George Mkuchika akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka Manispaa ya Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi kampeni ya Utatu itawezekana na Mfumo wa kuripoti matukio ya rushwa (Takukuru App) uliofanyika katika Viwanja wa Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.[/caption]Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amesema kuwa Serikali inatakeleza jukumu kubwa la kuleta usawa wa haki kwa wananchi nchini kwa kupambana na rushwa ikiwemo ufisadi ili kuleta maendeleo kwa wananchi, kwa hiyo Jeshi la Polisi linaunga mkono jukumu hilo ambalo linafanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
“ Mchakato wa kampeni hii ni sehemu ya matakwa ya kihistoria na kitaasisi katika jitihada za kupambana na rushwa nchini iliyoanzishwa chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa kifungu namba 11 ya mwaka 20007, sheria hii ilitungwa baada ya kufutwa kwa sheria ya kuzuia rushwa ya Takukuru sura 329 ambayo ilifanyiwa marejeo mwaka 2002, kwa hiyo katika kutekeleza majuku haya kampeni hii ambayo mchakato wake ulianza Novemba, 2017 leo inazinduliwa itasaidia sana kupunguza ajali barabarani”, Alisema IGP. Sirro.