Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mkemia Atumia Milioni 317 Kuimarisha Huduma za TEHAMA
Oct 11, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Ahmed Sagaff, MAELEZO


Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imetumia Shilingi milioni 317 kuimarisha huduma za TEHAMA kwa wananchi.

Leo jijini Dodoma, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amesema fedha hizo zimenunua vifaa vya kisasa 55.

“Mifumo hii imewezesha Mamlaka kupunguza matumizi ya karatasi na kusaidia upatikanaji wa majalada kwa urahisi, kuboresha usimamizi wa rasilimali fedha na kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa kiasi kikubwa.

“Aidha, imewezesha kurahisisha utoaji wa mizigo, hivyo kuimarisha biashara na kuchangia katika ukuaji wa uchumi, kurahisisha uandaaji wa bajeti, kuboresha usimamizi wa matumizi ya fedha za umma pamoja na usimamizi wa rasilimali watu mahali pa kazi”, ameeleza Dkt. Mafumiko.

Mifumo ya TEHAMA inayotumika sasa katika taasisi hiyo ni mfumo wa ukusanyaji mapato yasiyo ya Kodi Serikalini (Government electronic Payment Gateway - GePG), mfumo wa pamoja wa Ugomboaji Mizigo Bandarini (electronic Single Window System - eSWS), na mfumo wa Usajili na Utoaji Vibali kwa Wadau wa Kemikali (Customer Chemicals Management Portal - CCMP).

Mingine ni mfumo wa kielectroniki wa Ofisi (e-Office System), mfumo wa Bajeti (Planning and Reporting – PLANREP), mfumo wa Uhasibu wa Malipo Serikalini (MUSE) na mfumo wa mahudhurio (Biometric Attendance System).

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi