Wajumbe wa Mkutano Mkuu Kivuli wa Vijana wa Umoja wa Mataifa Zanzibar 2021, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi akizungumza kwa njia ya mtandao (hayupo pichani) mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, na kuwashirikisha Vijana mbalimbali, ukiwa na kauli mbiu “Fursa na Uwekezaji kwa Vijana katika Uchumi wa Buluu”
f
Rais wa Mkutano Mkuu wa Vijana Kivuli wa Umoja wa Mataifa Zanzibar 2021, Ndg. Ahmada Salum Suleiman akiongoza Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, unaozungumza Uchumi wa Buluu, ukiwa na kauli mbiu “Fursa na Uwekezaji wa Vijana katika Uchumi wa Buluu”
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Kivuli wa Umoja wa Mataifa Zanzibar 2021, Mwakilishi kutoka Canada Ndg. Adil Ali Bakari, akichangia wakati wa mkutano huo wa Vijana uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, ukiwa na kauli mbiu “Fursa na Uwekezaji wa Vijana katika Uchumi wa Buluu”
Mwakilishi kutoka Nchini Australia Ndg. Abdulsamad Suleiman akijibu hoja zilizoibuliwa na Wajumbe wa mkutano wa kwanza wenye sura ya Kimataifa Kivuli wa Umoja wa Mataifa Zanzibar 2021, uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar