Mke wa Rais wa Zanzibar Aongoza Wanamichezo Kufanya Mazoezi ya Viungo
Sep 24, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Mke wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mama Mariam Mwinyi akijumuika katika mazoezi ya viungo baada ya kumaliza matembezi ya Kilomita 5.5 yaliyoazia katika eneo la Regeza mwendo na kumalizika katika viwanja vya mpira Dole Wilaya ya Magharibi “A”Unguja kwa mazoezi ya pamoja ya viungo yaliyofanyika leo tarehe 24-9-2022. (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Majini Magharibi Unguja, Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana na Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid Mwita na (kushoto) ni Mkuu wa JKU, Kanali Makame Abdalla Daima
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe.Tabia Maulid Mwita akizungumza na Wanamichezo wa Vikundi vya mazoezi ya viungo wa Wilaya ya Magharibi “A”Unguja, baada ya kumaliza matembezi na mazoezi ya viungo katika viwanja vya mpira Dole, kabla ya kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi kuzungumza
Mke wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mama Mariam Mwinyi akizungumza na Wanamichezo wa vikundi vya mazoezi ya viungo wa Wilaya ya Magharibi “A” Unguja baada ya kumaliza matembezi ya Kilomita 5.5 na mazoezi ya pamoja ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya mpira Dole leo tarehe 24-9-2022.
Wanamichezo wa vikundi vya mazoezi ya viungo wa Wilaya ya Magharibi “A”Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mama Mariam Mwinyi wakati akizungumza na kutowa nasaha zake kwao baada ya kumaliza mazoezi ya pamoja ya viungo baada ya kumaliza matembezi ya Kilomita 5.5 yalioazia katika eneo la Regeza mwendo hadi viwanja vya mpira vya Dole leo tarehe 24-9-2022.