Mke wa Rais wa Zanzibar Akabidhi Vifaa vya Kilimo cha Mwani
Nov 07, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation "ZMBF", (kulia) akimkabidhi Mashine ya kusagia Mwani Mwenyekiti wa kikundi cha "Ukweli ni Njia Safi Bweleo" Wilaya ya Magharibi "B" Mkoa wa Mjini Magharibi, Bi. Safia Hashim Makame (katikati) wakati akiwa katika ziara ya kugawa vifaa vya Mwani leo, wengine kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Dimani, Mhe. Mwanaasha K.Juma na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi "B", Mhe Hamida Mussa Khamis,
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation "ZMBF",(wa pili kushoto) akimkabidhi mashine ya kuchanganyia juice ya Mwani Mwenyekiti wa kikundi cha "Ukweli ni Njia Safi Bweleo" Wilaya ya Magharibi "B" Mkoa wa Mjini Magharibi, Bi. Safia Hashim Makame (katikati) wakati akiwa katika ziara ya kugawa vifaa vya Mwani leo,wengine (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya Magaharibi "B", Mhe. Hamida Mussa Khamisi na (kulia) ni Mjumbe wa Bodi ya ZMBF", Dkt. Mwatima Abdalla Juma na Mwakilishi wa Jimbo la Dimani, Mhe. Mwanaasha K. Juma.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi ambaye pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation "ZMBF",(kushoto) akiangalia bidhaa mbalimbali za zao la mwani alipotembelea katika duka la kikundi cha "Ukweli ni Njia Safi Bweleo" (kulia) ni Mwenyekiti wa kikundi, Bi. Safia Hashim Makame akiwa katika ziara ya kugawa vifaa vya Mwani leo.