Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mitambo ya Kisasa Kutumika Kusafisha Maji Taka Dar
Jan 16, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_27155" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akizungumza mara baada ya kukagua mashine ya kusukuma Majitaka katika eneo la Msasani Jijini Dar es Salaam.

[/caption] [caption id="attachment_27156" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) Shabani Mkwanya wakati akikagua chemba za Majitaka katika eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ali Hapi amepongeza utendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam DAWASA na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya Maji Taka katika Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa Wananchi wanapata huduma Bora.

Akizungumza wakati wa ziara yakukagua maeneo yenye changamoto za majitaka na mradi wa uboreshaji wa huduma za maji taka ili kujionea hatua iliyofikiwa na DAWASA katika kutekeleza miradi hiyo Mhe. Hapi amesema kuwa ameridhishwa na kazi inayofanywa na Mamlaka hiyo katika Wilaya hiyo.

[caption id="attachment_27157" align="aligncenter" width="750"] Fundi wa DAWASCO akifunua chemba wakati Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi (mwenye suti nyeusi) akikagua chemba hiyo katika eneo la Msasani.
[/caption] [caption id="attachment_27159" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Modester Mushi akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni Ali Hapi kuhusu mradi wa ujenzi wa mtambo wa kusafisha Majitaka, Jangwani Beach, Dar es Salaam.[/caption]

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Mamlaka hiyo bomba lenye jumla ya kilomita 563 litajengwa ili kusafirishia maji taka hadi kwenye mitambo mikubwa itakayojengwa Mbezi beach, Jangwani na Kurasini jijini Dar es salaam.

Mtambo utakaojengwa eneo la Kilongawima utakuwa na uwezo wa kusafisha lita za ujazo 16,000 kwa siku na utajumuisha mfumo wenye urefu wa kilomita 97 utakojengwa katika eneo la mbezi Beach, Kawe, Tegeta na maeneo ya jirani na kutekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia na unatarajiwa kugharimu dola za Marekani milioni 65.

Mradi mwingine ni ule wa ujenzi wa mtambo wa kusafisha mita za ujazo 11,000 kwa siku utakaojengwa Kurasini ukihusisha maeneo ya Keko, Changombe, Kurasini, Temeke na Uwanja wa Taifa ambapo mfumo wake utakuwa na urefu wa kilomita 90.

[caption id="attachment_27154" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), Shabani Mkwanya, wakati akikagua mashine ya kusukuma majitaka, na mradi wa ujenzi wa mtambo wa kusafisha majitaka unatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DaresSalaam (DAWASA).[/caption]

Aidha, katika eneo la Jangwani mtambo wenye uwezo wa kusafisha lita za ujazo 200,000 kwa siku utajengwa ambapo mabomba yatalazwa kutoka Ubungo,Kinondoni, Mwanenyemala, Msasani, katikati ya Jiji na Ilala hadi Jangwani ambapo awamu ya kwanza ikikamilika itahusisha mtambo wa kusafisha kiasi cha lita za ujazo 25,000 za maji taka kwa siku.

Mradi huo katika eneo la Jangwani utagharimu dola za marekani milioni 90 ambapo taratibu za manunuzi zinaendelea ili kumpata mshauri na hatimaye mkandarasi, lengo ni kuanza kwa ujenzi huo mapema mwaka huu.

DAWASA imekuwa ikishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wakuu wa Wilaya katika kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi