Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Misri Yaonesha Nia Kuwekeza Biashara ya Nyama Nchini
Sep 11, 2023
Misri Yaonesha Nia Kuwekeza Biashara ya Nyama Nchini
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akisalimiana na Waziri wa Kilimo kutoka nchini Misri, Mhe. El Sayed El Kosayer walipokutana jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo kando ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika mwishoni mwa wiki.
Na Administrator

Katika jitihada za kufungua biashara hususan ya nyama inayotoka Tanzania kwenda nchini Misri, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega  amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo kutoka nchini Misri, Mhe. El Sayed El Kosayer ili kuona uwezekano na kuweka mazingira wezeshi ya biashara hiyo baina ya nchi hizo mbili.

 

Waziri Ulega alifanya mazungumzo hayo na Mhe. El Kosayer kando ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Kilimo kutoka nchini Misri, Mhe. El Sayed El Kosayer akimueleza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega kuhusu lengo la wao kuomba kukutana nae muda mfupi baada ya kukutana jijini Dar es Salaam kwa kando ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika mwishoni mwa wiki.

Pamoja na kujadiliana mambo mengine, suala la biashara ya nyama kutoka Tanzania kwenda kuuzwa nchini Misri lilijadiliwa kwa kina huku  Mhe. El Kosayer akiahidi kulifanyia kazi kwa haraka  ili biashara hiyo iweze kuleta matunda kwa pande zote mbili.

 

Mapema wakati wa mazungumzo yao, Mhe. Kosayer alimueleza Waziri Ulega kuwa lengo la kukutana kwao ni kuona namna wanavyoweza kuendelea kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi ili ziweze kuwanufaisha wananchi wa pande zote mbili.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi