Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Miradi 76 ya Utalii na Utamaduni Imeanzishwa Nchini-Mhe. Pindi Chana
Oct 08, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi  Dkt. Pindi Chana amesema jumla ya miradi 76 ya Utalii wa Utamaduni imeanzishwa katika Kanda za Kaskazini, Kusini na Kanda ya Ziwa ambazo zinaendelea kutangaza nchi ya Tanzania.

Amesema hayo Oktoba 07, 2022 jijini Arusha wakati akitoa salamu za wizara yake katika Uzinduzi wa Tamasha la Maasai Festival litakalofanyika mwaka  2023, ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikua Naibu Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na  Michezo  Mhe. Pauline Gekul.

"Wizara imetenga eneo la Makumbusho lililopo Dar es Salaam kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Utamaduni ikiwemo Mila, Desturi, vyakula, na mavazi," amesema Mhe. Chana.

Mhe. Chana ameongeza kuwa, Maasai Festival ni moja ya mazao ya Utalii wa Utamaduni ambayo yatasaidia kutangaza nchi vyema na kuongeza idadi ya watalii kutembelea vivutio vya nchi na kuongeza pato la Taifa.

Tamasha hilo ni miongoni mwa matamasha ambayo yanafanyika nchini kwa lengo wa kuhamasisha, kutangaza na kurithisha Utamaduni wa Watanzania.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi