Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mifumo ya WISN na POA kuraisisha kutambua uzito na wingi wa kazi katika vituo vya huduma.
Jun 11, 2018
Na Msemaji Mkuu

Muwezeshaji kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bw.Mfaume Hemedi akieleza faida za mfumo unaotumika kubaini mahitaji ya watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya(WISN) na ule unaotumika kupanga mgawanyo wa watumishi hao kulingana na uhitaji wa kila kituo (POA) kwa Waganga wakuu wa Halmashauri,Maafisa utumishi,Makatibu wa Afya na Maafisa utawala yalioanza leo Mkoani Iringa.Mifumo hiyo pia inasaidia kutambua uzito na wingi wa kazi uliopo katika vituo vya huduma na pia kupanga kwa kufuata vipaumbele vya watumishi katika vituo vya afya na zahanati.

Muwezeshaji kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bw.Mfaume Hemedi akionyesha kwa vitendo jinsi Mifumo ya WISN na POA inavyopanga  watumishi wa vituo vya afya na zahanati kulingana na uzito na wingi wa kazi leo mkoani Iringa.

Washiriki wa mafunzo ya mifumo ya kubaini mahitaji ya watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya(WISN) na ule unaotumika kupanga mgawanyo wa watumishi hao kulingana na uhitaji wa kila kituo (POA) wakifualia mafunzo mbalimbali leo mkoani Iringa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi