Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mhe. Mwakyembe: Stand United Hakikisheni Mnachukua Kombe la Ligi Kuu
Dec 13, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_24782" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimkabidhi jezi ya Timu ya Stand United kwa muanzilishi wa Timu hiyo Bw.Steven Masele (katikati)iliyotolewa na BIKOSPORTS kama sehemu ya udhamini (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji BIKOSPORTS Bw. Charles Mgeta.[/caption]

Na: Anitha Jonas – WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe  amewataka wachezaji wa Timu ya Stand United  kuchukua Kombe la Ligi Kuu .

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo alipokuwa katika mkutano wa kutangazwa kwa mdhamini wa timu hiyo ambaye ni BIKOSPORTS  aliyetoa udhamini wa Sh. Milioni Mia Moja pamoja na kununua jezi za wachezaji watakazo tumia katika msimu huu wa ligi.

[caption id="attachment_24783" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akishuhudia makabidhiano ya mfano wa hundi ya shillingi milioni mia moja kutoka kwa Mdhamini wa timu ya Stand United Mkurugenzi Mtendaji Bw.Charles Mgeta (wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Timu ya Stand United Dkt. Ellyson Maeja.[/caption]

“Soka la leo siyo kama la zamani linahitaji uwekezaji na pesa za kutosha kusaidia  kupata wachezaji wazuri wenye viwango vya juu,Makocha wenye uweledi  na mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kwa wachezaji,”Mhe.Dkt. Mwakyembe.

Naye Mweyekiti wa Timu ya Stand United Bw.Dkt. Ellyson Maeja alitoa shukrani kwa Kampuni ya Biko kwa udhamini huo na kuaahidi kutumia fedha hizo vizuri kwa manufaa ya timu ikiwa ni pamoja  kulipa mishahara ya wachezaji.

“Tunashukuru sana Biko kwa udhamini huu pia napenda kuwa hahikisha kuwa fedha hizi zitatumika vizuri pamoja na kuongeza chachu katika maendeleo ya timu ikiwemo kujituma kwa wachezaji wa timu na kuleta mafanikio makubwa katika msimu huu wa ligi,”Dkt.Mgeta.

Pamoja na hayo naye Mkurugenzi Mtendaji wa BIKO Bw.Charles  Mgeta alitoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza na kusaidia sekta ya michezo nchini kwa maendeleo ya taifa letu pia amewataka watanzania kuendelea kucheza bahati nasibu ya BIKOSPORTS sababu ni rahisi na unalipwa  kwa haraka.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi