Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Maandalizi Serengeti 2022 Yakamilika, Wasanii Onyesheni Umahiri Wenu- Mhe. Mchengerwa
Mar 09, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

 Na John Mapepele
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa Wasanii wote wa muziki watakaotumbuiza kwenye tamasha kubwa la historia la Serengeti Machi 12-13, 2022 jijini Dodoma kuonyesha umahiri wao ili kuutangaza utamaduni wa kitanzania duniani na kuliingizia taifa mapato.

Mhe. Mchengerwa amesema hayo leo Machi 9, 2022 ambapo amefafanua kuwa lengo la tamasha hilo pamoja na kutoa burudani ni kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia muziki wa Tanzania.

“Tumekusudia kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta zetu kwa kuzifanya ziwanufaishe wasanii wenyewe na Taifa kwa ujumla hivyo tamasha hili linakwenda kufungua Tanzania kwenye ngazi za kimataifa” amefafanua Mh.Mchengerwa

Amesema zaidi ya wasanii mia moja watakutanishwa  katika siku mbili na kuitikisa dunia kupitia tamasha hilo ambalo limeratibiwa na Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo.

Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amesema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri tayari kwa ajili ya burudani hiyo kabamnbe ambayo haijawahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.

“Niseme tu kwamba kila kitu kinakwenda vizuri, ni matarajio yetu watu watashiriki kikamilifu kwenye tamasha hili ambalo limeratibiwa kwa kiwango cha juu kabisa”. Ameongeza Dkt. Abbasi.

Amewataka wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla kushiriki ili kujionea vipaji na vipawa vya wasanii wa kitanzania.

Aidha Mhe. Mchengerwa amewataka wasanii watakaoshiriki kutambua kuwa dunia itakuwa ikiwafuatilia kupitia vyombo mbalimbali vya habari hivyo ni fursa ya kipekee ya kuonyesha uwezo wao ili waweze kunufaika na kazi zao.
Tayari wasanii mbalimbali wameshatua jijini Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya kutoa burudani kwenye tamasha hili.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi