Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mhe. Gekul Aiagiza BMT Kusimamia Mashirikisho ya Michezo Kufuata Kalenda ya Michezo
Nov 21, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Shamimu Nyaki

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul  ameliagiza Baraza la Michezo Nchini (BMT) kuhakikisha Mashirikisho yote yanayojihusisha na michezo yanaendesha mashindano yao kulingana na Kalenda ya Michezo.

Naibu Waziri Gekul ametoa agizo hilo katika hafla ya ufunguzi wa Mashindano ya Michezo kwa Mashirika ya Umma, Taasisi za Serikali na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) iliyofanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Novemba 20, 2022 jijini Tanga.

"Mhe. Makamu wa Rais naomba nikuhakikishie kwamba, Wizara kupitia BMT itaendelea kushirikiana na mashirikisho yote ya michezo, na kuhakikisha michezo inachezwa   mahali pa kazi na maeneo mengine" amesema Mhe. Gekul.

Ameongeza kuwa, wizara itaendelea kuhakikisha michezo katika ngazi zote inakua na Wananchi wanashiriki ili kuimarisha afya zao, kujenga upendo umoja na ushirikiano pamoja na  kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

Mashindano ya SHIMMUTA mwaka huu yanashirikisha takriban timu 52 zinazoshiriki michezo 12 na inaongozwa na  Kauli Mbiu ya " Michezo ni Fursa Tuitumie Vyema Kuimarisha Afya za Wafanyakazi kwa Uchumi Imara wa Taifa".

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi