Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mgalu : Siridhishwi na Kasi Mkandarasi wa Mradi wa REA, Kibondo Kigoma
Jul 11, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_45187" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akiwasha umeme katika moja ya sehemu za huduma za kinyozi wa kiume katika kijiji cha Nyange wilayani Kibondo mkoani Kigoma alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini( REA)[/caption]

Na Zuena Msuya, Kigoma

Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu,amesema haridhishwi na kasi ya usambazaji wa umeme vijijini inayofanywa na  mkandarasi wa Kampuni ya  Urban and Rural Engineering Services, wilayani Kibondo mkoani Kigoma.

Mgalu ametoa kauli hiyo,kwenye mkutano na wananchi  wakati  alipofanya  ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini wilayani humo  na kuwasha umeme katika kijiji cha Nyange.

Mgalu alisema kuwa, mkandarasi huyo amekuwa akitekeleza mradi huo kwa kusuasua na hivyo kusababisha hofu kwa wananchi pamoja na kuwakatisha tamaa kuwa  huenda mradi huo usikamilike  licha ya wananchi hao kujiandaa kuupokea.

Hata hivyo Mgalu aliongeza kuwa, mkandasi huyo tayari alikwisha lipwa fedha zake ili kutekeleza mradi huo na kwamba endapo atashindwa kutekeleza kwa muda uliopangwa basi sheria itachukuwa mkondo wake kulingana na mkataba.

[caption id="attachment_45184" align="aligncenter" width="960"] Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu( kushoto) akiteta jambo na Meneja wa Shirika la Umeme mkoani Kigoma, Mhandisi Masingija Lugata(kulia) wakati wa mkutano na wananchi wa kijiji cha Nyange hawapo pichani,Naibu Waziri alifika kijijini hapo kuwasha umeme na kukagua maendeleo mradi wa usambazaji umeme vijijini( REA)[/caption]

Sambamba na hilo amemtaka mkandarasi huyo kuwepo eneo la mradi muda wote,pia kuongeza nguvu kazi katika kutekeleza mradi huo.

Alifafanua kuwa Mkandarasi huyo anatakiwa kukamilisha mradi huo ifikapo mwezi Juni mwaka 2020 kwa kuunganisha  vijiji 40 katika wilaya ya Kibondo vilivyo umbali wa kilometa 283, lakini mpaka sasa ameunganisha vijiji 3 tu, na kusimamisha nguzo umbali wa kilometa 90 zililovutwa nyaya umbali wa kilometa 50 tu.

“Kasi ya mkadarasi huyu katika kutekeleza mradi wa usambazaji wa umeme vijijini hapa Kibondo hairidhishi kabisa, idadi ya vijiji vilivypo na vilivyounganishwa ndogo mno,pia anafanya kazi kwa kusuasua na akiendelea hivi serikali haitamvumilia itafanya maamuzi magumu, tunataka wananchi wote wapate umeme kwa wakati, fedha alishalipwa,” alisisitiza Mgalu.

Mbali ya kuwepo kwa changamoto hiyo, Mgalu aliwatoa hofu wananchi kwa kuwataka kutokata tamaa na kwamba waendelee kusuka nyaya katika nyumba zao kwakuwa  mradi huo utatekelezwa kama ulivyopangwa wote wataunganishiwa umeme.

Pia aliwasisitiza kuwa malipo ya kuunganisha umeme katika nyumba zao ni shilingi 27,000 tu na wasikubali kulipa zaidi na endapo itatokea mtu anadai fedha zaidi basi watoe taarifa sehemu husika ili watu hao waweze kushughulikiwa.

Vilevile  wananchi hao wasikubali kuuziwa vifaa vya umeme kama vile nguzo pamoja LUKU kwa kuwa vifaa hivyo hutolewa bure kwa wananchi wote.

[caption id="attachment_45185" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Lois Peter Bura, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyange hawapo pichani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika Wilaya ya Kibondo na kuwasha umeme katika kijiji cha Nyange.[/caption]

Kwa upande wake Meneja mradi wa kampuni ya ukandarasi ya Urban and Rural Engineering Services, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza sababu kubwa ilikuwa ni kukwama kwa vifaa bandarini.

Hata hivyo amesema kuwa sasa wamepata suluhisho hivyo muda wowote vifaa hivyo vitafika katika eneo la mradi na watanzaa kufanya kazi usiku na mchana kufidia muda waliopoteza.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Lois Peter Bura, amewataka wananchi wa Kibondo kuendelea kuilinda miundominu ya umeme iliyopo katika maeneo yao na kwamba mradi huo utatekelezwa kulingana na mkataba.

Vilevile amemtaka mkandarasi  kushirikiana na ofisi ya Wilaya na kueleza pale walipokwama ili kutatua changamoto zilizopo kwa manufaa ya wananchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi