[caption id="attachment_29057" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akisisitza jambo wakati wa mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Itwangi Wilaya ya Shinyanga alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA.[/caption] [caption id="attachment_29058" align="aligncenter" width="750"] Msimamizi wa Mradi wa REA Hussein Shemdasi, (kulia) akimtambulisha Mkandarasi wa Mradi wa REA Mkoa wa Shinyanga kutoka kampuni ya Angelic (kushoto).[/caption]
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu amewataka Wakuu wa Mikoa kuingiza Agenda ya Nishati katika vikao vya Maendeleo vya mikoa kwa kuwa sekta hiyo ni kichocheo kikuu cha sekta nyingine kiuchumi na kimaendeleo.
Aliyasema hayo wakati alipomtebelea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ofisini kwake wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji Nishati vijijini unaotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani humo.
[caption id="attachment_29059" align="aligncenter" width="750"] Meneja wa Tanesco Kanda ya Magharibi Macline Mbonile akieleza jambo wakati wa mkutano wa Naibu Waziri na wananchi wa kijiji cha Itwangi.[/caption] [caption id="attachment_29060" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (kulia) akimweleza jambo Mku wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati Naibu Waziri alipomtembelea ofisini kwake.[/caption]Aliongeza kuwa, ili sekta zote ziweze kuendelea zinahitaji nishati ya umeme hivyo imefika hatua ambayo masuala ya nishati ni muhimu yakapewa nafasi katika vikao hivyo vya maendeleo kwa kuwa ikiwa haitapewa nafasi inaweza kuchangia kupUnguza kasi ya maendeleo tarajiwa.
Aidha, akizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano ya hadhara katika vijiji vya Itwangi na Nyambui, Mgalu amesisitiza kuhusu Wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo kuhakikisha kuwa wanaripoti katika ofisi za Serikali kuanzia ngazi za Vijiji, Wilaya na Mikoa ili kuweka mazingira bora na rafiki ya utekelezaji ka wa miradi husika.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani humo kuwasilikiza wateja na kuhakikisha linasambaza nishati hiyo kwa wananchi wengi zaidi ikizingatia kuwa, mahitaji ya umeme hususani maeneo ya mijini yamekuwa makubwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josphine Matiro aliiomba wizara kuwafikiria wananchi ambao wako tayari kuchangia ili kupata huduma ya nishati hususan kwa walio katika maeneo ya pembezoni.
Naye Msimamizi wa Mradi wa REA Hussein Shemdasi, amewataka wananchi watakaounganishwa na huduma ya umeme kuutumia kwa uzalishaji ili kujiongezea kipato. Pia, alisisitiza kuhusu wakandarasi kushirikiana na viongozi wa Serikali ili kuwezesha mradi huo kutekelezwa kikamilifu.
Kwa upande wake, Meneja wa Tanesco Kanda ya Magharibi Macline Mbonile aliwataka wananchi kufanya maandalizi kipindi cha mradi ili wanapofikiwa wakati wa utekelezaji waweze kuunganishwa na huduma hiyo.