Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mfumuko wa Bei Washuka Kufikia Asilimia 5.4
Jul 10, 2017
Na Msemaji Mkuu

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akitoa taarifa ya mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2017 ambao umepungua hadi asilimia 5.4 toka asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Mei, 2017, kulia ni Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei wa ofisi hiyo Bi. Ruth Minja.

Na Mwandishi Wetu

Mfumuko wa bei umepungua hadi kufikia asilimia 5.4 mwezi June, 2017 ikilinganishwa na asilimia 6.1 ya mwezi Mei mwaka 2017.

Taarifa ya kushuka kwa mfumuko wa bei kwa kipindi cha mwezi mmoja imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo.

“Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2017 umepungua hadi asilimia 5.4 ikilingwanishwa na asilimia 6.1 mwezi June, 2017. Hii ina maana kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi June, 2017 imepungua zaidi ya ikilinganishwa na kasi iliyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2017,” alieleza Kwesigabo.

Hayo yanajiri ikiwa ni utaratibu wa ofisi hiyo ya takwimu kutoa takwimu kila mwisho wa mwezi kwa lengo la kudhibiti bei za bidhaa na mfumko wake kwa mtumiaji. Bwana Kwisegela amesema kuwa, makundi ambayo fahirisi za bei hufuatwa ni pamoja na vyakula na vinywaji baridi, nishati na mafuta pamoja na bidhaa na huduma zote za jamii.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikliza Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo wakati akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa mwezi Juni mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kwa kusema kuwa, mfumuko huo umepungua kwa sababu ya kushuka kwa baadhi ya bidhaa za vyakula huku akizitaja bihdaa hizo za chakula zilizoshuka bei, kuwa ni pamoja na mahindi kwa asilimia 5.1, unga wa mahindi kwa asilimia 2.4, unga wa mihogo kwa asilimia 5.7, maharage kwa asilimia 2.4, dagaa kwa asilimia 3.2, mbogamboga kwa asilimia 5.7 na viazi mviringo kwa asilimia 6.2.

Kwa upande mwingine Kwesigabo alisema kuwa mfumuko wa bei kwa bidhaa zisizo za vyakula na nishati kwa mwezi June, umeshuka hadi asilimia 1.9 kutoka ailimia 2.2 mwezi Mei, 2017.

Mkurugenzi huyo wa Takwimu alieleza kuwa faharisi inayotumika kukokotoa aina hiyo ya mfumuko wa bei, haijumuishi vyakula vinavyoliwa nyumbani na migahawani, vinywaji baridi, dizeli, gesi ya kupikia, mafuta ya taa, mkaa kuni na umeme.

Kwa mujibu wa Bwana Kwesigabo, mfumuko wa bei unaonesha kuwa kwa ujumla mfumuko wa bei ya bidhaa unaopimwa kwa kwa kipimo cha mwezi umepungua kwa asilimia 0.1 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.2 ilivyokuwa mwezi Mei, mwaka huu.

Kwa upande wa shilingi ya Tanzania katika manunuzi ya bidhaa mbalimbali umezidi kuimarika ikilinganishwa na mwezi uliopita abapo alisema. “Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidha na huduma umeimarika kidogo na kufikia shilingi 91 Na senti 66 mwezi June, 2017 ikilinganishwa na shilingi 91 na senti 53 ilivyokuwa mwezi, Mei, 2017.”

Kwa mujibu wa Bwana Kwesigabo, amesema kuwa, kupungua kwa mfumuko huo wa bei hauna tofauti kubwa sana na nchi za Afrika Mashariki ambapo mfumuko kama huo umepungua kwa mataifa ya Jumuiya hiyo, ambapo kenya mfumuko huo umepunpua kwa asilimia 9.12 na nchini  Uganda mfumuko huo umepungua kwa asilimia 6.4.

Ikumbukwe kuwa, mfumuko huu wa bei hutegemea Zaidi kupanda na kushuka kwa bidhaa za vyakula na vinywaji, bidhaa za nishati, bidhaa na huduma mbalimbali za kijamii pamoja na bidhaa zisizo za vyakula na vinywaji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi