Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kuleta maboresha makubwa katika mfumo mpya wa usimamizi wa fedha za umma
Jun 06, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Daudi Manongi,MAELEZO,IRINGA.

Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) umeelezwa kuleta maboresha makubwa katika mfumo mpya wa usimamizi wa fedha za umma ikiwemo kushushwa kwa mfumo hadi kwenye ngazi ya mtoa huduma. Hayo yameelezwa na Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw.Juma Shaha wakati akitoa mafunzo ya mfumo huo kwa wahasibu,waweka hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Iringa,Tanga na Morogoro leo Mkoani Iringa.

“Hivi sasa matumizi yote yanayofanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa vituo vyake vya Afya na Shule yatahifadhiwa na kuwekwa wazi kwa vituo vya kutolea huduma”,Aliongeza Bw.Shaha.

Aliongeza kuwa Maboresho mengine katika mfumo wa usimamizi wa fedha za umma katika tolea la 10.2 (Epicor 10.2) ni kwamba mifumo yote ya msingi ya usimamizi wa fedha katika sekta za umma kwa sasa itaweza kuwasiliana na kushirikishana taarifa ambapo hapo awali Mamlaka za Serikali za Mitaa walilazimika kupitia mipango na bajeti katika mfumo mmoja na hivyo kuleta ugumu katika uwajibikaji na ufanisi katika matumizi ya fedha za Serikali.

Kwa upande wake Mhasibu kutoka Mkoa wa Songwe Bw.David Johnson amesema kuwa Mfumo wa Epicor 10.2 utaunganishwa na mfumo unaowezesha mabenki kulipana kwa mfumo wa TISS ambao utaruhusu malipo yote kufanyika kwa njia ya kielektronikali na hivyo kuwezesha malipo kulipwa kwa uhakika na haraka na hivyo kupunguza gharama kwa Serikali ambapo hapo awali malipo yalikuwa yakifanyika kwa kutumia makaratasi n.k

“Mfumo huu utapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi kwani mfumo wake wa kielektoniki ni mzuri na utaleta ufanisi wa hali ya juu”,Aliongeza Bw.Johnson

Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni Mradi wa miaka mitano unaotekelezwa katika mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara. Mafunzo haya yanaendeshwa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Serikali ya Marekani kupitia Mradi wa USAID wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3). Mafunzo yatafanyika katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mtwara, Mbeya, Kagera na Mwanza.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi