Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma  Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuchochea Uwazi na Uwajibikaji
Jun 04, 2018
Na Msemaji Mkuu

Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya

Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa toleo la 10.2 (Epical 10.2 ) umetajwa kuchochea utekelezaji wa dhana ya uwazi, uwajibikaji na utawala bora katika usimamizi wa fedha za umma .

Akisoma hotuba  ya Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya,   Bi. Mariam Mtunguja, Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza  amesema kuwa mafunzo ya mfumo wa Epicor 10.2 yatasaidia kuongeza tija katika utendaji kutokana na mfumo huo kuandaliwa mahsusi kuungana na mifumo mingine ili kukidhi matakwa ya maboresho yanayofanywa katika usimamizi wa fedha za umma.

Mafunzo hayo yanawashirikisha wahasibu, maafisa ugavi, na waweka hazina wa mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa, na yanaendeshwa na Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kwa kushirikiana na Serikali ya Marekani kupitia Mradi wa Uimarishwaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3, unaosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani ( USAID), .

 Hivi sasa, Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini zitatumia mfumo mmoja wa uhasibu ujulikanao kama mfumo wa usimamizi wa Fedha za Umma, toleo la 10.2 utakaosaidia kuhakikisha kuna mfanano katika uhasibu,utoaji wa taarifa na usimamizi wa fedha.

“Mafunzo haya yana lengo la kuwajengea uwezo ili muweze kusimamia mapato na matunizi ya fedha za umma kwenye Halmashuri na pia kuwapatia uelewa wa mabadiliko ya msingi yaliyofanyika bila kukwamisha utoaji wa huduma kwa wananchi” Alisisitiza Ntigeza.

Akifafanua Bi.  Ntigeza amesema kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa watahakikisha kuwa  kuna matumizi sahihi  ya mifumo kuanzia ngazi za vituo vya kutolea huduma kuanzia mkoani hadi ngazi ya Halmashuri zote.

Aliongeza kuwa  awali maafisa katika maamlaka za Serikali za walilazimika kupitia mipango na bajeti katika mfumo mmoja, mapato katika mfumio mwingine na matumizi kwenye mfumo mwingine, hivyo kuleta ugumu katika uwajibikaji,ufanisi, na thamani ya fedha katika matumizi ya  fedha za Serikali.

Mfumo wa Epicor 10.2 utaunganishwa na mfumo unaowezesha malipo yote kufanyika kwa njia ya kielektroniki, Mfumo pia  unwezesha matumizi yote yanayofanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika vituo vya Afya na Shule kuhifadhiwa na kuwekwa wazi kwa vituo vya kutolea huduma pamoja na jamii  wanayoitumikia.

Kwa upande wake  Afisa Usimamizi Fedha kutoka  Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Mmaka Mwinjaka amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuongeza uwazi , uwajibikaji na upatikanaji wa taarifa kwa wakati hivyo kuondoa ubadhilifu.

Aliongeza kuwa EPICA 10.2 ni mfumo ulioboreshwa ili kuweza kuongea na mifumo mingine kama ile ya ukusanyaji mapato na ule wa kupanga bajeti, mipango na kutoa ripoti yani PlanRep.

Kuanzia Julai 2018, Serikali ya Tanzania itaanza kutumia mfumo mpya wa uhasibu kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa 185 za Tanzania bara, Mradi wa Uimarishji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni Mradi wa miaka  mitano unaotekelezwa katika mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara. PS3 inafanya kazi katika sekta mbalimbali ili kuimarisha mifumo ya mawasiliano,  utawala bora, fedha na rasilimali watu, hususani kwa jamii zenye uhitaji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi