Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mchengerwa Afika Uturuki Kuongeza Hamasa Mashindano Kombe la Dunia
Oct 03, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 3, 2022 amewasili mjini Istanbul-Uturuki kwa ajili ya ziara ya kikazi na pia kufuatilia Mashindano ya Kombe la Dunia kwa watu wenye ulemavu yanayoendelea nchini humo.

Mhe. Mchengerwa amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Lt. Gen. Yacoub Mohamed na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi ambaye alitangulia.

Akizungumza mara baada ya kuwasilili, ameipongeza timu ya Tembo Warriors kwa kuifunga Uzbekistan goli 2-0 kwenye mechi iliyopigwa leo Oktoba 3, 2022 katika uwanja wa TFF RIVA.

“Nawapongeza Tembo Warriors na watanzania wote waishio nchini Uturuki kwa kuleta hamasa kubwa katika mashindano haya. Tanzania inaweza na tukiacha uvivu  tutafika mbali na ushindi huu ni wa watanzania wote”, alisema Mhe. Waziri Mchengerwa.

Aidha, amempongeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi kwa kuhakikisha timu inakuwa sawa kisaikolojia na pia kuhamasisha hamasa katika mechi zote za mashindano.

“Wizara yetu haina jambo dogo, sisi kila jambo ni kubwa na tutahakikisha Tanzania haitobaki nyuma katika mchezo wowote ule” alisema.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi