Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mchakato wa Uanzishaji Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi Waanza.
Jul 21, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_7158" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete akisisitiza jambo alipokuwa akifungua warsha kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.[/caption]

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano - Sekta ya Mawasiliano, Injinia Angelina Madete amesema uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ufundi (ICoT), utasaidia kupunguza pengo lililopo sasa  baina ya wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo hapa nchini.

Akifungua warsha ya wataalam washauri na wadau wa Taasisi ya Teknolojia ya Ufundi Jijini Dar es salaam leo, Mhandisi Madete amewataka wataalam hao kufanya uchambuzi wa kina ili kuwezesha taasisi hiyo mpya kukidhi mahitaji ya  mafundi sanifu na mchundo  na hivyo kukidhi uwiano wa kimataifa unaotaka mhandisi mmoja, fundi sanifu watano na mafundi mchundo 25.

[caption id="attachment_7159" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Taasisi ya ECOM Research Group Ltd, Profesa Godwin Daniel Mjema akifafanua jambo mbele ya wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.[/caption] [caption id="attachment_7161" align="aligncenter" width="750"] Mratibu wa wataalam wa uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), Profesa Peter Chonjo akiwasilisha mada namna ambavyo ICoT inaweza kuanzishwa mbele ya wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha ya siku moja kuhusu uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.[/caption] [caption id="attachment_7160" align="aligncenter" width="750"] Mratibu wa wataalam wa uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), Profesa Peter Chonjo akiwasilisha mada namna ambavyo ICoT inaweza kuanzishwa mbele ya wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha ya siku moja kuhusu uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.[/caption]

“Tunataka kuwa nchi ya viwanda vya kati ifikapo mwaka 2025, hivyo ni lazima tuwe na wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo wa kutosha watakaofanyakazi kwa weledi na kumudu ushindani katika soko la ajira”, amebainisha Injinia Madete.

Mhandisi Madete amesema kuwa pengo la wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo limeongezeka kutokana na vyuo vingi vya kati kutoa shahada hivyo uwepo wa ICoT utakabiliana na kumaliza changamoto hiyo.

Aidha amezungumzia umuhimu wa taasisi hiyo mpya kuanzisha kozi ya waendesha mitambo ambayo mahitaji yake ni makubwa hapa nchini na kwa sasa hakuna chuo kinachotoa kozi hiyo.

[caption id="attachment_7162" align="aligncenter" width="750"] Mmoja wa wataalam elekezi wa uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), Profesa Beatus Kundi akifafanua jambo kwa wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha ya siku moja kuhusu uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.[/caption] [caption id="attachment_7165" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya Ujenzi, Mhandisi John Ngowi (wa pili kulia) akifuatilia mada wakati wa warsha ya siku moja kuhusu uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete.[/caption] [caption id="attachment_7168" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete(wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya ujenzi mara baada ya kufungua warsha ya siku moja kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo. (Na: Mpiga Picha Wetu)[/caption]

Hakikisheni taasisi hii inapata ithibati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), ili kuwawezesha wahitimu wote wa ICoT kupata fursa za kujiendeleza na elimu ya juu.

Naye mratibu wa wataalam wa uanzishaji ICoT Profesa Peter Chonjo amesema wamejipanga kuhakikisha taasisi hiyo ya teknolojia ya ujenzi inakuwa ya mfano hapa nchini kwa kuwa itawezesha wataalam wengi wa ujenzi kuwa na weledi unaokubalika na kuibua uwezo wa ushindani katika soko la ajira na hivyo kuwezesha Tanzania kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

 Tanzania inakadiriwa kuwa na mtandao wa barabara wenye zaidi ya kilometa elfu 87 na kati ya hizo elfu 35 ni barabara za kitaifa na elfu 52 ni barabara za Wilaya ambazo ujenzi wake unahitaji wataalam wa kutosha katika fani ya ujenzi na uendeshaji wa mitambo.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi