Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mazungumzo Kufanyika Kuhusu Vikao vya Bunge Kutangazwa Mbashara
Feb 14, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi Wetu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amewaeleza Waandishi wa Habari kwamba muhimili huo utazungumza na wadau mbalimbali kuhusu hoja ya vikao vya Bunge hilo kutangazwa mbashara na vyombo vya habari.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo (Februari 14, 2022) alipokutana na wanachama 23 wa Jukwaa la Wahariri Tanzania na Waandishi wa Habari 40 wanaoripoti taarifa za Bunge.

“Niseme hivi hili ni jambo ambalo linazungumzika na acha tujaribu kuona sababu zilizofanya wakati ule liwepo na sasa hivi lisiwepo na tutazungumza na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari halafu tuone namna ya kulifanyia kazi.

“Halafu na nyinyi kama Waandishi wa Habari lazima tutahitaji mawazo yenu kwa sababu wakati mwingine Bunge kuwa mbashara ni hoja nzuri lakini ni lazima utazame pia kitu gani kinaenda mbashara kwa wananchi.

“Nafikiri ni mambo ambayo sisi tunaweza kushauriana na kwa maana ya kama Bunge, upande wa Serikali lakini na nyinyi kama wahusika kwa sababu hasa nyinyi kama Waandishi wa Habari sio kila kitu kinaripotiwa kama habari.

“Kwa hivyo nafikiri ni jambo ambalo tutatakiwa kufanya kazi kwa pamoja halafu tuone tunalifanyiaje kazi jambo hili,” ameeleza Mheshimiwa Spika.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi