Matukio ya Uapisho wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Picha
Nov 09, 2020
Na
Msemaji Mkuu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya hafla fupi ya Uapisho wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi leo tarehe 09 Novemba 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi muda mfupi baada ya kumuapisha leo tarehe 09 Novemba 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi muda mfupi baada ya kumuapisha leo tarehe 09 Novemba 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi watatu kutoka (kulia), Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma wapili kutoka (kulia), Spika Job Ndugai watatu kutoka kushoto, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakwanza kushoto, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson wapili kutoka kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge wakwanza kulia pamoja na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mara baada ya hafla fupi ya Uapisho wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 09 Novemba 2020. PICHA NA IKULU