Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio ya Picha Wakati AICC Ikizindua Ukumbi wa Kisasa Jijini Arusha
Jul 23, 2017
Na Msemaji Mkuu

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), Balozi Dkt. Ladislaus Komba mara baada ya Waziri kusoma hotuba ya Uzinduzi wa Ukumbi mpya wa Kisasa wa Lake Nyasa. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), Balozi Dkt. Ladislaus Komba, akitoa neno la utangulizi wakati Kituo hicho cha Mikutano kilipozindua Ukumbi wake mwingine mpya wa kisasa wa Lake Nyasa. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akisalimiana na Mjumbe Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), Goddard James wakati Waziri akiwasili katika Uzinduzi wa Ukumbi mpya wa Kisasa wa Lake Nyasa. Katikati mwenye suti nyeusi ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Elishilia Kaaya. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akisalimiana na Mjumbe Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), Ali Mzee Ali wakati Waziri akiwasili katika Uzinduzi wa Ukumbi mpya wa Kisasa wa Lake Nyasa. Kushoto kwa  Waziri ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Elishilia Kaaya na kulia kabisa ni Mkujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AICC, Goddard James. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akitembelea maonesho ya Wajasiliamali yaliandaliwa na Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) ikiwa ni sehemu ya Uzinduzi wa Ukumbi mpya wa Kisasa wa Lake Nyasa. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akisalimiana na mmoja wa washiriki wa maonesho ya Wajasiliamali yaliandaliwa na Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) ikiwa ni sehemu ya Uzinduzi wa Ukumbi mpya wa Kisasa wa Lake Nyasa. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (wa nne kushoto walio kaa) akiwa katika picha ya pamoja na Bodi wa Wakurugenzi pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) baada ya kuzindua Ukumbi mpya wa Kisasa wa Kituo hicho wa Lake Nyasa. Kushoto mkwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Fabian Daqarro.

Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Elishilia Kaaya, Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Eliakim Samwel, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Amandajune Donald na Mkurgenzi wa Huduma za Hospitali, Profesa Sendui Ole Nhuyaine wakifurahi jambo kabla ya uzindua Ukumbi mpya wa Kisasa wa Kituo hicho wa Lake Nyasa. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), Balozi Dkt. Ladislaus Komba baada ya Waziri kuzindua Ukumbi mpya wa Kisasa wa Lake Nyasa. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Jijini Arusha. 

(Picha zote kwa Hisani ya AICC)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi