Matukio katika Picha: Ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Mbagala
Dec 17, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Msimamizi wa Kituo cha Kusambaza Umeme cha Mbagala, Mhandisi Neema Ngogo (wa pili kulia) , akimuonyesha Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (wa pili kushoto) namna ambavyo umeme unapokelewa, kupozwa na kusambazwa kituoni hapo, wakati wa ziara ya kutembelea kituo hicho Jijini Dar es salaam, Desemba 16, 2021.
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (kulia) akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Shirika la Umeme (TANESCO), Wilaya ya Mbagala pamoja na wasimamizi wa Kituo cha Kusambaza Umeme cha Mbagala, wakati wa ziara ya kutembelea kituo hicho Jijini Dar es salaam, Desemba 16, 2021.
Msimamizi wa Kituo cha Kusambaza Umeme cha Mbagala, Mhandisi Neema Ngogo( wa pili kulia) , akimuonyesha Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (wa pili kushoto) namna ambavyo umeme unapokelewa, kupozwa na kusambazwa kituoni hapo, wakati wa ziara ya kutembelea kituo hicho Jijini Dar es salaam, Desemba 16, 2021.
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (kulia) akizungumza na Uongozi wa Shirika la Umeme (TANESCO), Wilaya ya Mbagala pamoja na wasimamizi wa kituo cha kusambaza Umeme cha Mbagala, baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Kituo hicho, Jijini Dar es salaam, Desemba 16, 2021.