Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio katika Picha: Ziara ya Kitaifa ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Mji wa New Delhi nchini India
Oct 09, 2023
Matukio katika Picha: Ziara ya Kitaifa ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Mji wa New Delhi nchini India
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima wakati wa hafla ya mapokezi yake katika viwanja vya Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi nchini humo tarehe 09 Oktoba, 2023.
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Serikali ya India wakati wa mapokezi yake katika viwanja vya Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi nchini humo tarehe 09 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akijibu swali lililoulizwa na Waandishi wa Habari kuhusu mategemeo ya ziara yake nchini India tarehe 09 Oktoba, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wakati wakielekea kwenye mazungumzo katika Jengo Maalum la kupokelea wageni wa Kitaifa Hyderabad House New Delhi Nchini India tarehe 09 Oktoba, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi mara baada ya kuwasili katika Jengo Maalum la kupokelea wageni wa Kitaifa Hyderabad House New Delhi Nchini India tarehe 09 Oktoba, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na ujumbe wake akiwa na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi katika mazungumzo Rasmi katika Jengo Maalum la kupokelea wageni wa Kitaifa Hyderabad House New Delhi Nchini India tarehe 09 Oktoba, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari katika Jengo Maalum la kupokelea wageni wa Kitaifa Hyderabad House New Delhi Nchini India tarehe 09 Oktoba, 2023.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi