Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio katika picha ziara ya Kamati ya Uongozi ya MKURABITA mkoani Njombe
Jan 28, 2021
Na Msemaji Mkuu

Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Katarina Revoati, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wamyonge Tanzania (MKURABITA) leo Januari 28, 2021 walipomtembelea ofisini kwake.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA, Bw. Haji Janabi (wa tatu kulia), akieleza jambo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Katarina Revocati. Wengine ni wajumbe wa Kamati hiyo na watendaji wa MKURABITA
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA na watendaji mbalimbali wa taasisi hiyo, wakiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Katarina Revocati (wa pili mbele kulia) mbele ya Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Kulia kwake, ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel ole Njoolay na Makamu Mwenyeki wa Kamati, Bi. Emmaculata Sanje. Kulia Mratibu wa MKURABITA ambaye pia ni Katibu wa Kamati, Dkt. Seraphia Mgembe.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA, Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel ole Njoolay (kushoto), akieleza jambo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Katarina Revocati, wajumbe wa Kamati hiyo walipomtembelea ofini kwake mkoani Njombe leo Januari 28, 2021.

(Picha zote na MAELEZO)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi