Matukio Katika Picha: Waziri Mhagama Akagua Utekelezaji wa Miradi ya Nyumba za Makazi za NSSF Dar Es Salaam
Sep 23, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Mmoja wa wapangaji wa nyumba za NSSF eneo la Dungu Wilaya ya Kigamboni Dar es Salaam, Bi. Flora Mwakipesile akieleza uzuri wa nyumba hizo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara kukagua maendeleo ya mradi huo.
Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi Nssf, Bw. Gabriel Silayo akimweleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake katika Miradi ya nyumba za NSSF eneo la Mtoni Kijichi Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na timu aliyoambatana nayo kukagua mradi wa nyumba za makazi za NSSF eneo la Mtoni Kijichi Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika miradi yua nyumba za makazi za NSSF eneo la Mtoni Kijichi, Toangoma na Dunge Jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Masha Mshomba.