Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akihutubia washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini Jijini Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi .
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula akihutubia washiriki wa wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini Jijini Dodoma ambapo Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) alikuwa mgeni rasmi .
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akisisitiza kuhusu fursa zilizopo Mkoani Dodoma wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dustan Kitandula akizungumzia manufaa ya kuanzishwa kwa Tume ya Madini wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume hiyo Jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki Kuzindua Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula wakati akimkabidhi vitendea kazi mara baada ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi vitendea kazi Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof. Shukrani Manya mara baada ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga ( kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Aderladus Kilangi( kulia) Wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya madini leo Jijini Dodoma.
Makamishana wa Tume hiyo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi Vitendea kazi mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo Dkt. Florence Turuka ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamishna wa Tume ya Madini mara baada ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki wakati wa hafla ya kuzindua Tume hiyo iliyofanyika leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Anjelina Mabula akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kuandikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.
( Picha zote na Frank Mvungi )