Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio katika Picha: Msigwa Afanya Ukaguzi Mradi wa Upanuzi wa Usikivu wa Redio ya TBC Taifa na Bongo FM
Feb 25, 2026
Matukio katika Picha: Msigwa Afanya Ukaguzi Mradi wa Upanuzi wa Usikivu wa Redio ya TBC Taifa na Bongo FM
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha, ametembelea na kukagua mradi wa upanuzi wa usikivu wa Redio ya TBC Taifa na Bongo FM unaotekelezwa katika eneo la Ngarenanyuki, wilayani Arumeru, Arusha. Msigwa amekagua mradi huo leo Februari 25, 2026, unaotekelezwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, hatua inayolenga kuongeza usikivu na huduma bora za utangazaji kwa wananchi.
Na Administrator

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi