Matukio katika Picha: Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo
Sep 01, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiteta na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga kabla ya kufungua mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ulioanza leo Septemba 1, 2022.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwa na Naibu Makatibu Wakuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama (Mazingira) na Bw. Abdallah Hassan Mitawi (Muungano) kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo kwa ulioanza leo Septemba 1, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar kabla ya kufungua kufungua mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ulioanza leo Septemba 1, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali kabla ya kufungua Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ulioanza leo Septemba 1, 2022.