Matukio katika Picha: Makamu wa Rais Katika Kilele cha Wiki ya Ubunifu Mei 19
May 19, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa mbunifu wa gari linalotumia umeme Masoud Kipanya wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo tarehe 19 Mei 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Funguo Innovation kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Joseph Manirakiza wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo tarehe 19 Mei 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Dkt. Philip Mpango akimkabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa mshindi wa ubunifu, Arqhm Isihaka Adam kutoka Shule ya Msingi Mikumi Mpya Morogoro aliyebuni kengele ya nyumbani inayotumia sauti na mwanga kwa ajili ya watu wote ikiwemo wenye mahitaji maalum wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo tarehe 19 Mei 2022.Kushoto ni Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, kulia ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na washiriki pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo tarehe 19 Mei 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza mtoto Ethan Kaganda aliyebuni mfumo wa kutoa taarifa iwapo wanafunzi zaidi ya mmoja wameingia katika choo kimoja kwa wakati mmoja ili kuepusha wenye nia ovo wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo tarehe 19 Mei 2022
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza mtoto Tanya Gorecha aliyebuni mifumo mbalimbali ya umeme wakati wa kilele cha Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa Mwaka 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo tarehe 19 Mei 2022.