Matukio katika Picha: Makamu wa Rais Ahudhuria Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani
Jul 08, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akicheza mchezo wa Bao na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya walioshiriki Maadhimisho Siku ya Kiswahili Duniani yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa mratibu wa Mradi wa Programu ya Urithi na Ukombozi wa Bara la Afrika, Boniface Kadili wakati alipokagua mabanda mbalimbali ya walioshiriki Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea tuzo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akishuhudia utiaji Saini wa makubaliano baina ya Tanzania na Afrika Kusini juu ya ufundishaji wa lugha ya Kiswahili nchini Afrika Kusini wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Kamusi Maalum kwa ajili ya Shule za Msingi pamoja na mkakati wa Taifa wa kubidhaisha ndani na nje ya nchi wa mwaka 2022-2032 wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi baadhi ya vitabu vya lugha ya Kiswahili Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika Kusini, Prof. Matsie Angelina Motshekga wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.