Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Day 2: Matukio katika picha Mafunzo ya usimamizi wa fedha za umma kwa watumishi wa mikoa na mamlaka za Serikali za mitaa leo Mkoani Iringa.
Jun 05, 2018
Na Msemaji Mkuu

Mhasibu kutoka Mkoa wa Songwe Bw.David Johnson akifundisha jinsi ya kufanya malipo mbalimali kwa kutumia mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma ujulikanao kama Epicor 10.2 kwa wahasibu na Maafisa usimamizi wa Fedha wa Mikoa leo Mkoani Iringa.

Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw.Juma Shaha akielezea jinsi gani mfumo wa usimamizi wa fedha za umma ujulikanao kama Epicor 10.2 utakavyounganishwa na mabenki na kufanya malipo yote kwa njia ya kielektroniki na pia na kuwezeshana kulipana kwa urahisi leo Mkoani Iringa.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Morogoro Bw.Gasper Francis akiongoza kikao cha wahasibu na Maafisa usimamizi wa Fedha wa Mikoa wakati wa mafunzo ya kutumia mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma ujulikanao kama Epicor 10.2 mkoani Iringa leo.

Washiriki wa Mafunzo ya Usimamizi wa fedha za Umma ambao wanajumuisha wahasibu na Maafisa usimamizi wa Fedha wa Mikoa mbalimbali wakifuatilia mafunzo hayo leo Mkoani Iringa.

  Washiriki wa Mafunzo ya Usimamizi wa fedha za Umma ambao wanajumuisha wahasibu na Maafisa usimamizi wa Fedha wa Mikoa mbalimbali wakifuatilia mafunzo hayo leo Mkoani Iringa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi