Matukio katika Picha: Maandalizi ya Uzinduzi wa Matokeo ya Sensa
Oct 25, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Na Mwandishi Wetu - Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Bw. Kaspar Mmuya Oktoba 25, 2022 ameongoza Kikao cha Kamati Tendaji inayohusisha Makatibu Wakuu kwa ajili ya Maandalizi ya Uzinduzi wa Matokeo ya Kwanza ya Sensa ya Watu na Makazi utakaofanyika Oktoba 31,2022 Katika Uwanja Wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Katika uzinduzi huo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Takwimu, Bi. Ruth Minja akitoa taarifa ya mwongozo wa uzinduzi huo utakavyofanyika wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia kikao hicho
Baadhi ya Makatibu wa Wakuu wakifuatilia hoja za kikao hicho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael, katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba, na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi.
Mratibu wa Sensa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Adela Mpina akitolea ufafanuzi baadhi ya taarifa zilizowasilishwa za maandalizi ya Uzinduzi huo.