Matukio katika Picha: Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru
Dec 09, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama kwenye Maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika leo tarehe 09 Desemba 2021 katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,akisalimiana na kuwapongeza Watanzania kwa kutimiza miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, katika Maadhimisho yaliyofanyika leo tarehe 09 Desemba 2021 katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakionesha baadhi ya zana mbalimbali za Kivita pamoja na kazi mbalimbali wanazofanya katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo tarehe 9 Desemba, 2021.
Vikosi mbalimbali vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vikipita Kikakamavu na kuonesha shughuli mbalimbali wanazozifanya mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo tarehe 9 Desemba, 2021.