Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Kuwasilishwa Kwa Taarifa za Kamati Maalum za Uvuvi wa Bahari Kuu na ile ya Gesi Asilia
Jun 02, 2018
Na Msemaji Mkuu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akizungumza mara baada ya kupokea na kumkabidhi Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ambaye ni Kaimu Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni  taarifa za Kamati Maalum za Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi Asilia leo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Naibu Spika akitoa maelezo ya awali kuhusu  Kamati Maalum za Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi Asilia leo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuwasilishwa kwa taarifa hizo.

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ambaye ni Kaimu Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni akizungumzia hatua zitakazochukuliwa na Serikali mara baada ya kupokea taarifa ya  Kamati Maalum kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kuchunguza  Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi Asilia leo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati  Maalum ya kuchunguza Gesi  Asilia Mhe. Dastan  Kitandula akitoa muhutasari wa taarifa ya Kamati hiyo katika hafla yakukabidhi taarifa hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza Gesi  Asilia Mhe. Dastan  Kitandula akiwasilisha taarifa ya Kamati hiyo kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai katika hafla iliyofanyika  viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.

Mwenyeki wa Kamati Maalum ya Uvuvi Bahari Kuu Mhe. Anastazia Wambura akisitiza umuhimu wa rasimali za bahari katika kuchangia pato la Taifa wakti akiwasilisha taarifa ya Kamati hiyo wakati wa hafla iliyofanyika  viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.

Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji Tanzania Major. General Richard  Makanzo akiteta jambo na  Kamishna wa  Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Bw. Nsato Marijani wakati Kamati Maalum za Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi Asilia zikiwasilisha taarifa zake leo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akimkabidhi Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ambaye ni Kaimu Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni taarifa ya Kamati ya Gesi Asilia wakati wa hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.

Mwenyeki wa Kamati Maalum ya Uvuvi wa Bahari Kuu  Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  taarifa ya Kamati  hiyo wakati wa hafla iliyofanyika katika viwanja vya Bunge leo.

Sehemu ya wabunge wakifuatilia hafla ya kukabidhiwa kwa taarifa ya Kamati Maalum ya Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi  Asilia wakati wa hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Gesi Asilia mara baada ya kuwasilishwa kwa taarifa za Kamati hiyo na ile ya Uvuvi wa Bahari Kuu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi