Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Hafla ya Kukabidhi Eneo la Ujenzi wa Kituo cha Umahiri Mpanda
Jul 15, 2018
Na Msemaji Mkuu

Mkurugenzi wa Sheria Kutoka Wizara ya Madini Bw. Edwin Igenge (Kulia) na Kaptain Jackson Stephano Muwakilishi kutoka Suma JKT wakitiliana saini kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Umahiri kwa kampuni ya SUMA JKT ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) wenye lengo la kusaidia kuwaongezea ujuzi wachimbaji wadogo, Mkoani Katavi katika Wilaya ya Mpanda.

 Mkurugenzi wa Sheria Kutoka Wizara ya Madini Bw. Edwin Igenge (Kulia) na Kaptain Jackson Stephano Muwakilishi kutoka Suma JKT wakibadilishana mikataba  baada ya utiaji saini kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Umahiri kwa kampuni ya SUMA JKT ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) wenye lengo la kusaidia kuwaongezea ujuzi wachimbaji wadogo, Mkoani Katavi katika Wilaya ya Mpanda.

 

Mkurugenzi wa Sheria Kutoka Wizara ya Madini Bw. Edwin Igenge (Kulia) na Msanifu Majengo kutoka kampuni ya Y&P Bw. Benjamin Kasiga (kushoto) wakimkabidhi Muwakilishi wa Kampuni ya SUMA JKT Kapteni Jackson Stephano mchoro kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) wenye lengo la kusaidia kuwaongezea ujuzi wachimbaji wadogo, Mkoani Katavi katika Wilaya ya Mpanda.

Wawakilishi kutoka Wizara ya Madini, SUMA JKT na Kampuni ya Y&P wakiangalia mchoro kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) wenye lengo la kusaidia kuwaongezea ujuzi wachimbaji wadogo, Mkoani Katavi katika Wilaya ya Mpanda

 

Eneo utakapotekelezwa mradi wa  Ujenzi wa Kituo cha Umahiri kwa kampuni ya SUMA JKT ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) wenye lengo la kusaidia kuwaongezea ujuzi wachimbaji wadogo, Mkoani Katavi katika Wilaya ya Mpanda.

(Picha na Hassan Silayo- MAELEZO - Mpanda)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi