Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanayowashirikisha Maafisa Ugavi wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Rukwa na Songwe kama wanavyoonekana wakifuatilia hafla ya kufunga mafunzo hayo leo yaliyofanyika kwa siku mbili Jijini Mbeya.
Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais,Tawala la Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Malowa Hamimu akizungumzia umuhimu wa maafisa ugavi kuzingatia mafunzo ya mfumo wa Epicor 10.2 wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo Jijini Mbeya Leo ambapo yaliwashirikisha maafisa hao kutoka mikoa ya Songwe, Mbeya, Njombe, Rukwa na Katavi
Afisa ugavi kutoka halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga Bw. Martin Sanane ambaye alikuwa mwenyekiti wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanayowashirikisha maafisa ugavi wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Rukwa na Songwe akizungumzia wajibu wa maafisa hao katika kutumia mfumo huo wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku mbili Jijini Mbeya. Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais,Tawala la Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Malowa Hamimu akisitiza umuhimu wa kuzingatia taratibu zinazotakiwa katika kutumia mfumo wa Epicor 10.2 kwa maafisa ugavi wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Rukwa na Songwe akizungumzia wajibu wa maafisa hao katika kutumia mfumo huo kabla ya hafla ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku mbili Jijini Mbeya
Afisa Ugavi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Bw. Godfrey Sanga akieleza faida za mfumo wa Epicor 10.2 mara baada ya hafla ya kufunga mafunzo kwa maafisa ugavi wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Rukwa na Songwe akizungumzia wajibu wa maafisa hao katika kutumia mfumo huo yaliyofanyika kwa siku mbili Jijini Mbeya.
(Picha zote na Frank Mvungi MAELEZO, Mbeya )