Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuajiri Maafisa Ugani 1,487
Nov 10, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_22247" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Azzan Zungu akiingia bungeni tayari kuongoza Mkutano wa tisa wa kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_22248" align="aligncenter" width="800"] Wabunge wakiwa wamesimama wakati wa dua ya kuiombea nchi na bunge wakati wa Mkutano wa tisa wa kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.[/caption]

Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma
Serikali imepanga kuajiri maafisa Ugani 1,487 katika mwaka wa Fedha 2017/2018 ili kuziba pengo la upungufu wa wataalamu hao kote nchini na kuongeza tija katika uzalishaji kwenye sekta ya Kilimo.
Akijibu swali la mbunge wa Nanyamba Mhe. Abdalla Chikota wakati wa Kipindi cha maswali  na majibu  Bungeni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. George  Mkuchika amesema kuwa kati ya mwaka 2013/2014 hadi 2016/2017 jumla ya Maafisa Ugani 5,710 waliajiriwa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
[caption id="attachment_22249" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Capt(Mst) George Mkuchika akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa Tisa wa kikao cha nne cha Bunge hilo leo Mkoani Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_22250" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso akijibu hoja mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.[/caption]
“Serikali imekuwa ikitoa vibali vya ajira za Maafisa Ugani katika Mamlaka za Serikali ya Mitaa kila mwaka wa fedha kutegemea uwezo wa bajeti” Alisisitiza Mkuchika.
Akisisitiza  Mhe.  Mkuchika amesema kuwa Serikali inatambua upungufu wa Maafisa Ugani hasa katika Halmashauri mpya  na Miji na itahakikisha inawapeleka Maafisa hao ili kuleta uwiano kati ya Halmashuri Kongwe na zile mpya.
[caption id="attachment_22251" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akijibu hoja mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_22252" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Hamisi Kigwangalla akijibu hoja mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.[/caption]
Aliongeza kuwa Wizara yake itashirikiana na Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa udahili katika vyuo vya Ugani unaongezeka ili idadi ya wataalamu hao iongezeka kulingana na mahitaji.
Katika Kukuza na kuongeza tija Katika Sekta ya Kilimo  Serikali imeweka mkazo katika kuongeza ujuzi na maarifa ya Wataalam wa Kilimo ili kuendana na dhana ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda.
[caption id="attachment_22253" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe.Stanslaus Nyongo akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali za wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_22254" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati Mhe.Subira Mgalu akitoa maelezo ya maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_22255" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe.Dk.Mary Mwanjelwa akijibu hoja mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi