Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Bungeni leo
Apr 20, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_30719" align="aligncenter" width="796"] Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo ya wabunge mapema leo Bungeni mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.[/caption] [caption id="attachment_30718" align="aligncenter" width="794"] Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akisisitiza kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi kuendelea kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao kote nchini leo Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.[/caption] [caption id="" align="aligncenter" width="826"] Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akitoa maelezo kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa kila kipande cha ardhi hapa nchini kinapimwa ili kuchochea maendeleo wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_30724" align="aligncenter" width="900"] Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Kagera Mhe. Oliver Semuguruka akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kuhusu maboresho yanayopaswa kufanywa katika sekta ya afya ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi katika Mkoa wa Kagera na katika hosipitali zote za umma.[/caption] [caption id="attachment_30720" align="aligncenter" width="894"] Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakifutilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.[/caption]

Picha na Frank Mvungi

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi