Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akizungumzia umuhimu wa kutunza rasilimali za Taifa kwa maslahi ya kizazi hiki na kijacho wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka 2018/2019 leo Bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge wa Muheza Mhe. Balozi Adadi Rajabu akizungumzia mchango wa sekta ya madini wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha ya Wizara ya Madini leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Singida Mhe. Martha Mlata akizungumzia umuhimu wa hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kulinda rasilimali madini wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka 2018/ 2019.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki akitoa hotuba ya kufunga maonesho ya madini yaliyofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wakala wa Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) Bw. Octavian Minja akisisitiza jambo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea maonesho ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa maonesho ya madini yaliyofanyika katika viwanja vya Bunge wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Madini wakati akifunga maonesho hayo leo Jijini Dodoma.
Mmoja wa washiriki wa maonesho ya madini yaliyofanyika katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Bi Susie Kennedy akifurahia jambo na Waziri wa Madini wakati akikabidhiwa cheti cha ushiriki wakati wa hafla yakufunga maonesho hayo leo Jijini Dodoma.
Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma leo.
Sehemu ya mabanda ya maonesho ya Madini kama inavyoonekana katika picha ndani ya Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
( Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)