Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mataifa Makubwa Waridhishwa na Ufafanuzi wa Serikali Kuhusu Shutuma za Baraza la Usalama.
Sep 15, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_13847" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Korea ya Kaskazini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na Mwandishi Wetu.

Serikali leo imekutana na mabalozi wa nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kutoa ufafanuzi rasmi kuhusu taarifa ya Baraza hilo inayoishutumu Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazoiwezesha Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa dhidi yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Augustine Mahiga amesema mabalozi wa nchi hizo ambazo ni China, Marekani, Russia, Ufaransa na Uingereza  wamefurahishwa na kuridhishwa na ufafanuzi huo.

[caption id="attachment_13848" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Korea ya Kaskazini, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Aziz Mlima na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara hiyo Bi. Mindi Kasiga.[/caption]

Katika mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Mahiga aliwaeleza waandishi wa habari kuwa wakati wowote kuanzia leo Serikali itawasilisha Umoja wa Mataifa taarifa yake rasmi kujibu shutuma hizo.

“Nitasafiri kesho (Jumamosi) kwenda New York kwa vikao vya kawaida vya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Natarajia taarifa yetu nikifika itakuwa nayo imeshafika huko lakini zaidi nikiwa huko nitatoa ufafanuzi kwa kirefu na natarajia kuonana na baadhi ya mabalozi na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa baadhi ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama kueleza jambo hilo” alieleza.

Balozi Dk. Mahiga aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Serikali ilipokea rasmi taarifa hiyo jana na kuielezea kuwa ilikuwa ‘imepitwa na wakati’ kwa kuwa Serikali kwa nyakati tofauti imekuwa ikuchukua hatua mbalimbali kutekeleza maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu vikwazo dhidi ya nchi hiyo.

“Hatuna ugomvi na Korea ya Kaskazini bali tunapinga utengenezaji, majaribio na matumizi ya silaha za nuklia na ndio maana tukapunguza sana mahusiano yetu na nchi hiyo” alisema Balozi Dk. Mahiga na kuongeza kuwa ndio sababu Tanzania inakubaliana na hatua zote za Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hiyo.

Pamoja na kuunga mkono na kutekeleza maazimio ya Umoja wa Mataifa, Dk. Mahiga alisema Tanzania ingependa kuona kuwa suala hilo linatafutiwa ufumbuzi kwa njia za mazungumzo rai ambayo inaungwa mkono na nchi nyingi katika Umoja wa Mataifa.

  [caption id="attachment_13849" align="aligncenter" width="750"] Mwandishi wa Habari toka kituo cha Televisheni cha Channel Ten, David Ramadhan akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (aliye kaa katikati) wakati Waziri huyo akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Korea ya Kaskazini.Picha na Eliphace Marwa.[/caption]

Kuhusu nini hatma ya shutuma hizo dhidi ya Tanzania, Balozi Mahiga amesema kwa sasa kinachotakiwa ni Serikali kutoa taarifa ya hali halisi ilivyo na kwamba hakuna tishio lolote la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua dhidi ya Tanzania.

“Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatutaka tutoe taarifa inayolingana na hali ilivyo sasa kwani hata mabalozi niliokutana nao baada ya mazungumzo yetu wameonesha kukubali kuwa hawana taarifa sahihi” Alisema Balozi Mahiga.

Katika kutekeleza hilo alibainisha kuwa Serikali inatakiwa kuthibitisha kama kweli hivi sasa wataalamu wa Korea Kaskazini bado wapo nchini na kueleza hali ya uhusiano kati ya Tanzania na nchi hiyo ilivyo sasa.

Kama unavyoona “wanatoa fursa kwetu tujieleze na hawajaonesha dalili zozote za kuchukua hatua dhidi yetu” alisema Balozi Dk. Mahiga na kusisitiza kuwa Tanzania ilianza kuandaa taarifa yake mara tu ilipopata taarifa hiyo rasmi jana (Alhamisi).

Akifafanua kuhusu madai hayo na utekelezaji wa maazimio ya Umoja wa Mataifa, Balozi Dk. Mahiga alitoa mfano wa hatua ya serikali ya kufuta usajili wa meli za nchi hiyo na kusitisha matumizi ya bendera ya Tanzania katika meli hizo.

Kuhusu ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama, Dk. Mahiga alibainisha kuwa suala hilo limesitishwa tangu mwaka 2014 lakini kwa kuwa linahusu mikataba utekelezaji wake unakwenda hatua kwa hatua.

Wakati huo huo, Balozi Mahiga amewataka watanzania kuwa watulivu na kwamba Serikali yao inatambua na kuamini kuwa amani na utulivu wa dunia ni sehemu ya utulivu na amani ya Tanzania na kusisitiza kuwa kitendo cha Tanzania kupinga silaha za maangamizi ni sehemu ya kulinda usalama wetu na kusisitiza kuwa “Tanzania haina uhasama na taifa lolote. Sisi ni wadau wa amani na usalama

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi