Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

"Mashujaa" wa Kichina Reli ya TAZARA Wakumbukwa
Apr 05, 2018
Na Msemaji Mkuu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiongea mbele ya viongozi wa Serikali na maafisa wa Ubalozi wa China nchini, wakati kumbukumbu ya Mafundi Wataalamu kutoka China waliofariki wakati wa ujenzi wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kati ya mwaka 1970-1976. Sherehe za kuwakumbuka zimefanyika leo katika makaburi hayo yaliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. (Picha na MAELEZO).

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. , akiweka maua katika moja ya makaburi ya Mafundi Wataalamu kutoka China waliofariki wakati wa ujenzi wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kati ya mwaka 1970-1976. Sherehe za kuwakumbuka zimefanyika leo katika makaburi hayo yaliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. (Picha na MAELEZO)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akipata maelezo kuhusu Mafundi Wataalamu kutoka China waliofariki wakati wa ujenzi wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kati ya mwaka 1970-1976. Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke. Sherehe za kuwakumbuka zimefanyika leo katika makaburi hayo yaliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. (Picha na MAELEZO)

Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke, akiweka maua katika moja ya makaburi ya Mafundi Wataalamu kutoka China waliofariki wakati wa ujenzi wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kati ya mwaka 1970-1976. Sherehe za kuwakumbuka zimefanyika leo katika makaburi hayo yaliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. (Picha na MAELEZO)

Baadhi ya wazee walioshiriki ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushiriki kumbukumbu ya Mafundi Wataalamu kutoka waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli hiyo kati ya miaka ya 1970-1976. Kutoka kushoto ni Martini Siwingwa (70), Simon Magohu (67), Ernest Fundi Kitahula (63), Mohamed Omar (68) na Ediferick Juma (64). Sherehe za kuwakumbuka zimefanyika leo katika makaburi hayo yaliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. (Picha na MAELEZO).

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akielezea historia ya ujenzi wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wakati kumbukumbu ya Mafundi Wataalamu kutoka China waliofariki wakati wa ujenzi wa reli hiyo kati ya mwaka 1970-1976. Sherehe za kuwakumbuka zimefanyika leo katika makaburi hayo yaliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. (Picha na MAELEZO).

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akisaini kadi maalumu kuwakumbuka Mafundi Wataalamu kutoka China waliofariki wakati wa ujenzi wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kati ya mwaka 1970-1976. Sherehe za kuwakumbuka zimefanyika leo katika makaburi hayo yaliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. (Picha na MAELEZO)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi